Halmashauri ya jiji la Arusha imeokoa zaidi ya shilingi milioni mia tatu
sitini na nne zilizokuwa zitumike kwa ajili ya kuwapa wakandarasi kwa
ajili ya kujenga madarasa baada yake kamati za shule kupewa jukumu la
kusimamia ujenzi wa madarasa hayo badala ya mkandarasi
Hayo yamebainishwa na meya wa halmashaur i ya jiji la Arusha Kalist Lazaro
wakati akiongea na waandish I wa habari ambapo alisema kuwa halmashauri
yake wamekaa chini na kuona kuliko fedha hizo zipewe wakandasi ili wajengee
madarasa ni bora fedha za ujenzi wa madarasa zipelekwe katika kamati za
shule pamoja na bodi za shule ili wasimamie ujenzi huo
Alisema kuwa sasa ivi halmashauri imetoa shilingi bilioni moja laki nne
kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 56 ya shule za msingi na fedha zote
zilishapelekwa katika kamati za shule ili waweze kusimamia ujenzi mpaka
ukamilike.
“zamani tulikuwa tunatumia wakandarasi kwa kutangaza tenda kwa ajili ya
kujenga madarasa ya shule za msingi ,lakini tangu tuanze kujenga madarasa
kwa kupitia kamati za shule na sio wakandarasi tumekuwa tunaokoa milioni
mia tatu sitini nne ambazo tumeziokoa tungetumia wakandarasi zote
zingeingia katika mfuko wa mkandasi sasa ndio maana tumeamua kumtumia kamati
za shule kwa shule za msingii “alisema Kalist
Aidha alisema kuwa jiji la Arusha kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto
ambao wanaandikishwa darasa la kwanza tuofauti na mwaka huliopita kwani
tangu zoenzi limeanza adi kufikia sasa wameshaandikisha wanafunzi wa darasa
la kwaza zaidi ya elfu 12000 tofauti na mwaka uliopita 2016 ambapo watoto elfu
tisa mia sita na mia waliandikishwa kuingia darasa la kwanza , ambapo
alisema bado wanaendelea kuandikisha watoto adi mwezi march ili watoto wote
waweze kwenda shule
Alisema kuwa kutokana na kuwepo na watoto wengi waliojiandikisha kumekuwa
na upungufu wa madarasa hivyo halmashauri imejenga madarasa 56 kwa ajili
ya watoto hao wapya na kukarabati madarasa manne ya shule ya msingi ambayo
yatasaidia kabisa kumaliza tatizo hili,ambapo alisema kuwa pia madarasa
hayo yanaitaji madawati na hadi sasa halmashauri imeshatoa fedha kwa ajili
ya madawati 1380 ambayo watoto hao watakalia katika madarasa hayo mapya
hivyo wanaimani kuwa watoto wote wanaoanza darasa la kwanza wataingia
madarasani na kukaa katika madawati na kusoma vizuri kama vile
inavyotakiwa.
Akifafanua kuhusu wanafunzi wa shule za sekondari alisema kuwa jiji la
Arusha lilifaulisha kwa asilimia 92% wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza
na kukakuwepo na upun gufu wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi hao lakini
jiji limeshajipanga vyema na imeanza kujenga madarasa 25 kwa ajili ya shule
za sekondari na kiasi cha shilingi milioni 700 zimeshatumwa katika bodi za
shule hizo na wanaimani adi ifike mwisho wa mwezi huu wanafunzi wote
waliofaulu kuingia kidato cha kwanza wataingia madarasani na kuendelea na
masomo kama kawaida.
“napenda ku sema kuwa hakuna mtoto ambaye amefaulu kuingia kidato cha
kwanza ataacha kuingia darasani ifikapo mwisho wa mwezi huu madarasa
yatakuwa tayari na wanafunzi wote waliofaulu wataenda shule “alisema kalist
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia