Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto),
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), Mkuu wa
Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi (wa tatu kushoto), Katibu Tawala wa mkoa wa
Dodoma, Rehema Madenge, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano
(wa pili kulia), Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel, Arindam Chakrabarty (kulia)
wakipiga makofi baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza,
katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akipongezana
na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia) baada
ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza mjini Dodoma jana. Kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi, Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma,
Rehema Madenge (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice
Singano (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel, Arindam
Chakrabarty (kulia).
Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto)
akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya
Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya
Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Meneja Uendeshaji kutoka kampuni ya Airtel Tanzania,Bwa.Asupya Naligingwa akitoa maelekeo mafupi namna ya kutumia huduma hiyo mpya ya Timiza wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza,
katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso
akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya
Nyerere Square, mjini Dodoma jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Airtel, Beatrice Singano.
Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso
wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya
Nyerere Square, mjini Dodoma jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Airtel, Beatrice Singano.
Pichani shoto ni Mmoja wa Waimbaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya Africans Star a.k.a Twanga Pepeta,Msafiri Diof akiwa sambamba na skwadi zima la madansa wa bendi hiyo wakitumbuiza mbele ya sehemu ya umati wa watu wakati wa uzinduzi wa huduma
mpya ya Airtel Money Timiza,uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Skwea, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa Waimbaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya Africans Star a.k.a Twanga Pepeta,Msafiri Diof akitumbuiza mbele ya sehemu ya umati wa watu wakati wa uzinduzi wa huduma
mpya ya Airtel Money Timiza,uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Skwea, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Bendi ya Twanga Pepeta wakiwa na wadau wengine wa Airtel katika Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya
Nyerere Square, mjini Dodoma jana
.Kikundi cha Ngoma za asili kutoka mjini Dodoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya
Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
baada ya huduma ya Airtel Money Tmiza kuzinduliwa,zikifuata shangwe kutoka kwa wageni waalikwa kama hivi pichani.
Pichani shoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi akijimwaya mwaya jukwaani wakati wa uzinduzi rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza,
katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.pichani kati ni Katibu Tawala wa mkoa wa
Dodoma, Rehema Madenge.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya
Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Baadhi ya Wasanii kutoka nyumba ya vipaji THT,wakitumbuiza mbele ya sehemu ya umati wa watu (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma
mpya ya Airtel Money Timiza,uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Squea, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
======= ====== =======
·
Airtel Money Timiza, huduma mpya inayotoa mkopo wa muda mfupi kwa wateja wake kwa njia ya simu za mkononi
·
Mikopo ya masharti rahisi inayotoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo kuweza kukuza kibiashara zao.
Dodoma Novemba 9 2014:
Airtel Tanzania leo imezindua huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel
Money kupata mkopo kwa njia ya simu zao za mkononi
kupitia Airtel Money.
Huduma hiyo imezinduliwa leo rasmi na Airtel
Tanzania kwa ushirikiano na AFB ambayo ni kampuni ya Kiafrika iliyobobea
katika huduma ya kutoa mikopon rahisi. Huduma hii nchini Tanzania
itajulikana kama "Airtel Money Timiza" ambapo lengo
lake ni kuungana na serikali katika kuwezesha wanannchi na wateja wa
Airtel wote kujipatia mikopo ya haraka na ya muda mfupi kwa marejesho
nafuu ya siku 7 hadi 28.
Akizungumza wakati wa uzinduzi,
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda alisema:"Uwezekano wa
wananchi kuweza kupata mkopo wa muda mfupi ni motisha kubwa kwa
wafanyabiashara wadogo na wakati hapa nchini .Kwa Airtel kushughulikia
hitaji hili muhimu la wananchi , ni jambo la muhimu kwani
wametuunga mkono serikali katika kutimiza mkakati yetu ya kuinua kipato
cha wajasiriamali na kuwahamasisha kuweza kujiendeleza kibiashara. Ni
dhahiri kwa upande mwingine, itasaidia kuchochea maendeleo ya kiuchumi
hapa nchini"
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso
alisema: “Leo uzinduzi wa huduma yetu ya Airtel
Money Timiza unadhihirisha dhamira ya dhati ya Airtel ya kutoa
huduma iliyo bora na nafuu ili kugusa maisha ya kila siku ya wateja
wetu hapa Tanzania . Tunaamini huduma hii itaongeza kasi ya ukuzaji wa
uchumi miongoni mwa makundi mbalimbali ikiwa
ni pamoja na vikundi vya wanawake, wajasiriamali na watu binafsi.
Pia
tunaamini kwamba mikopo hii ya Airtel Money Timiza itakuwa kichochea
cha upatikanaji wa huduma za mikopo kwa idadi kubwa ya wakazi waishio
mbali na huduma za banki na hivyo kuwasaidia
sana kuweza kumudu mahitaji yao ya muda mfupi na muda mrefu."
Kwa upande wake Muanzilishi wa afb Bw, Andrew Watkins-Ball alisema
“hii ni huduma ya mikopo ya
kipekee tofauti na benki ambayo mara nyingi mteja hulazimika kuwa na
historia ya uwekaji na utoaji katika banki hiyo, lakini mikopo ya afb
inatolewa kutokana na jinsi ambavyo mteja anatumia
simu.
Kwa hiyo sasa wateja wa Airtel watapata fulsa hii ya kupata
mikopo ya papo kwa hapo kwa kuwa tu wateja wakudumu na waaminifu kwa
Airtel. Hii itawasaidia sana watanzania kwa mara ya kwanza kupata msaada
wa haraka wa kifedha kwa haraka na nafuu, Ni imani
yangu itasaidia kubadilisha mfumo wa maisha kwa watanzania wengi wenye
uhitaji’
Akitoa ufafanuzi kuhusu huduma ya Airtel Money Timiza, Meneja bidhaa wa Airtel Money Bw, Moses Alphonce alisema “Airtel Money
Timiza ni huduma ya kipekee, kutokana na urahisi, ni huduma
iliyozingatia mahitaji ya kina kabisa ya mkopaji kwa kuondoa baadhi
masharti ambayo mara nyingi yamekuwa yakikwamisha wateja kupata msaada
wa haraka wa mkopo ili kujikimu”.
Ili
mteja aweze kupata mkopo hakikisha tu namba yako imesajiliwa na huduma
ya Airtel Money na anapaswa uwe umetumia huduma ya Airtel Money kwa
kipindi
cha siku 30, kisha piga *150*60 # na kuchagua TIMIZA ili ujichagulie
kiasi unachotaka kukopa kulingana na mahitaji yako au kulipa mkopo.
Mkopo
wa Airtel Money Timiza utatakiwa kulipwa ndani ya siku 28 kutoka
kwenye akaunti yako ya Airtel Money kama mteja mkopaji ulivyojulishwa
siku
alipokopa mkopo wake.
Huduma
ya Airtel Money ni salama na rahisi ambayo inawawezesha wateja kutuma
na kutoa fedha kati ya simu moja ya mkononi na kwenda nyingine katika
mitandao yote , kununua muda wa maongezi kwa ajili yako au ndugu jamaa
na marafiki. Na pia inampa uhuru mteja kuweza kulipa bili na vile vile
kununua bidhaa popote alipo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia