Hatimaye Rapa Rashidi Makwiro, maarufu Chid Benz,leo
amefanikiwa kupata dhamana na kutolewa rumande na kurejea uraiani.
Anatakiwa kufika mahakamani Novemba 11 ambapo kesi yake itatajwa tena.
Chid Benz 'King Kong' kutoka kundi la La familia Ilala, mchana wa October 28 alisimamishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Mashtaka matatu yanayomkabili Chid Benz ni;-
- Kukutwa na madawa na vifaa vya kutayarishaji uvutaji wa madawa
- Kusafirisha madawa ya kulevya
- Utumiaji wa madawa ya kulevya