TANZANIA SASA KUTUMIA NISHATI YA JOTO ARDHI ILI KUPUNGUZA TATIZO LA UKOSEFU WA NISHATI MARA KWA MARA

TANZANIA inatarajia kutumia nishati ya joto ardhi ambapo nishati hiyo
itaweza kusaidia maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya Viwanda pamoja na
kilimo ambapo pia nishati hiyo itakuwa ni ya kudumu.

hataivyo uwepo wa nishati joto hiyo hapa nchini utaweza kuruhusu uzalishaji
kuongezeka kwa kasi tofauti na sasa ambapo wakati mwingine shuguli za kila
siku zina simama kutokana na ukosefu wa nishati mbadala

kauli hiyo imetolewa na Naibu Kamisha wa Nishati mbadala Edward Ishengoma
wakati akiongea na wadau wa joto ardhi ambao wanapewa mafunzo pamoja na
mbinu mbalimbali za kitaalamu za joto ardhi.

Ishengoma alisema kuwa uzoefu kwa nchi ambazo zimeshaanza kutumia nishati
hiyo ya joto ardhi unaonesha kuwa wameweza kupiga hatua sana kwenye masuala
ya maendeleo na hivyo basi kama Tanzania itatumia nishati hiyo  nayo
itaweza kukua kiuchumi kwani kazi nyingi za uzalishaji zinategemea sana
Nishati.

Alitaja nchi ambazo mpaka sasa zimeshatumia Nishati hiyo ya Joto ardhi kuwa
ni nchi ya Ethiopia, pamoja na nchi ya kenya na hivyo sasa nayo Tanzania
itaaanza kutumia nishati hiyo ambayo tafiti zimeonesha kuwa nishati hiyo
ipo.

Aliongeza kuwa uwepo wa nishati hiyo hapa nchini utaweza kusaidia hata
kuongezeka kwa mambo mbalimbali hususani kwenye sekta ya uchumi, lakini pia
hata kwa wawekezaji ambao nao wataweza kufanya kazi zao kwa kuwa nishati
itakuwepo itakuwa ni ya kudumu kwani nishati hiyo ikishawekwa imeweka na
haikatiki ovyo kwani wakati wa uwekaji watatumia bomba la urefu wa kilomita
mbili na nusu hadi tatu kwenda kwenye miamba tofauti na nishati nyingine.

"Nishati ndio kila kitu hapa nchini sasa uwepo wa nishati hii utasaidia
sana tanzania kuweza kupanuka zaidi na sisi tunachokitaka ni kuwa
watanzania sasa wajue kuwa kuna kitu kama hiki lakini pia waweze kujua kuwa
nchi yetu imepita katika bonde la Afrika ya Mashariki kwa hiyo lazima
tutanufaika"aliongeza Ishengoma.

Awali Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela aliongeza
kuwa Serikali ina mkazo mkubwa sana wa kuendeleza nishati kwa watanzania
kwani tafiti zinaoenesha kuwa ili umaskini uweze kutoweka ni lazima kuwepo
na nishati

Mbali na hayo Mongela alisema kuwa nishati hiyo ya joto ardhi ipo sehemu
nyingi mfano katika maeneo ya Engaruka, lakini pia katika eneo la Natron
hivyo basi kuna umuhimu wa sekta husika kuhakikisha kuwa wanajifunza kwenye
kama Kenya, lakini pia Ethiopia ambazo tayari wameshatumia teknolojia ya
joto ardhi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post