KAMPUNI YA PAN AFRICAN ENERGY YATOA MSAADA WA MIFUKO 1500 YA SARUJI KWA WILAYA YA KILWA

Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Pan African Energy, Andrew Kashangaki (kwanza kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Peter Malekela (kulia) msaada wa saruji 1,500 yenye thamani ya shilingi milioni 18 kwa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Lindi ili kuwezesha ujenzi wa maabala 59 katika shule zake za sekondari zipatazo 24. Pembeni wanaoshuhudia ni viongozi wa halmashauri hiyo na wafanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Pan African Energy. Makabidhiano hayo yalifanyika mwanzoni mwa wiki Novemba 17, 2014 katika kiwanda cha Saruji cha Kilwa, Lindi. (Picha zote na Cathbert Kajuna.)
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya Peter Amosi Malekela akizungumza machache.
Waandishi wa habari wakifanya mahojiano na mwalimu wa masomo ya sayansi wa shule ya sekondari Mtanda ambapo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa na viongozi toka kampuni ya  Pan African Energy (T) Ltd.
Moja ya Maabala inayojengwa kwa msaada wa Pan African Energy (T) Ltd.
Moja ya mradi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa kwa msaada wa kampuni hiyo.
Moja ya Hospitalli ya Nangurukuru ikiwa imekwosha tayari kwa
Mazungumzo ya hapa na pale.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Peter Malekela (kulia) akiongea na wageni wake waliomtembelea ofisini kwake.
Msafara ukielekea eneo la tukio.
Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa na viongozi toka kampuni ya  Pan African Energy (T) Ltd wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Kampuni ya uchimbaji wa gesi ya Pan African Energy imetoa msaada wa mifuko 1500 ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 18 kwa halmashauri ya wilaya ya Kilwa ili kuwezesha ujenzi wa maabala katika shule zake za sekondari.
Akikabidhi msaada huo Andrew Kashangaki, Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa kampuni hiyo alisema wao wametoa msaada huo ili kuweza kutimiza lile agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuzitaka kila shule za sekondari kuwa na maabala ifikapo Novemba 30, 2014.
“Kampuni yetu imewekeza huku hivyo ni vyema kuendeleza eneo ambalo limewekeza ikiwa ni kutoa huduma kwa jamii inayotuzunguka likiwemo suala la elimu bora na afya kwa ujumla ndiyo maana umeona leo tumekabidhi msaada wa mifuko hii ya saruji,” alisema Bw. Kashangaki.
Bw. Kashangaki alisema kampuni yao, mbali na Aliongeza kuwa mbali na utoaji wa msaada huo, kampuni ya Pan African Energy alishajenga hospitali katika eneo la Nangurukuru ambao imekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa huko.
Pia alishukuru halmashauri ya Wilaya hiyo kwa uaminifu iliyouonyesha kwa kuanza kutumia saruji hizo kama zilivyokusudiwa.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa, Peter Malekela aliishukuru kampuni hiyo kwa kile walichotoa ambacho kwa kiasi kikubwa kimesaidia kuleta maendeleo katika wilaya yao jambo linaloleta faraja kwa wananchi.
Bw. Malekela alisema saruji waliyoipata waliigawanya kwa shule 24 za wilaya hiyo ambazo jumla ya maabala 59 zinahitaji, ambapo shule ya Kikanda, Kandawale, Miguruwe, Kiranjeranje, Nakiu, Likawale, Kikole, Pande, Mtanga, Njinjo, Namayuni, Kibata hizi zote zinahitaji maabala tatu (3) na mgao wa mifuko 76 ya saruji kila moja.
Nyingine ni shule ya sekondari Miteja, Mpunyule, Matanda, Songosongo, Dodomezi, Kivinje, Mibuyuni, Kipatimu, Alli Mchumo, Migumbi, Kijumbi hizi nazo zinahitaji maabala 2 kila moja na zinapata mgao wa mifuko 51 kila moja. Shule ya mwisho ni Kila yenyewe inahitaji maabala moja na imepata mgawo wa mifuko 25 ya saruji.
“Kila tunapopita tumekuwa mabalozi wenu wazuri kusema yale mazuri ambao mmekuwa mkiyafanya kwa wilaya yetu, tokea kampuni hii imeingia maendeleo ya eneo hili yanaonekana tofauti na zamani. Tunawaomba muendelee na moyo huu wa kujitolea na tunaalika makampuni mengine yaje tuijenge Kilwa yetu,” Alisema Bw. Malekela.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post