KILIMANJARO
serikali Mkoani Kilimanjaro imetoa agizo kali kwa wakurugenzi watendaji
wa halmashauri za wilaya za mkoa huo, kutokubadilisha
fedha za miradi ya maendeleo na kuzipeleka katika ujenzi wa maabara.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama , katika kikao cha
kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), ambapo aliwaonya wakurugenzi hao kutafuta njia
mbadala za kujenga maabara na sio kutumia fedha za miradi ya maendeleo.
Amesema
ujenzi wa maabara usizuie shughuli
zingine za miradi ya maendeleo kushindwa kukamilishwa huku akisisitiza kuwa miradi yote inayotekelezwa
katika halmashauri hizo ikiwemo, barabara, Maji, Afya na Kilimo ikamilishwe kwa
wakati kam ambavyo imepangwa.
Aidha Gama
amesema hata mvumilia Mkurugenzi atakaye bainika kuhamisha fedha za miradi ya
maendeleo na kuzipeleka katika ujenzi wa maabara na badala yake aliwataka
wakurugenzi hao kutafuta mbinu ambazo zitawawezesha kukamilisha maabara hizo
kwa wakati.
Kwa upande wake Kaimu afisa elimu mkoa,
Estomih Makyara amesema mkoa huo unakabiliwa na ukosefu wa maabara 333, ambazo
hadi sasa hazijaanza kujengwa.
Amefafanua kuwa
mkoa wa Kilimanjaro unajumla ya shule za sekondari za serikali 217, na kwamba
maabara zinazohitajika 651.
Aidha
aliongeza kuwa maabara zilizopo ni 154,
sawa na aslimia 23.7, zinazoendelea kujengwa pamoja na umaliziaji wake ni
maabara 169 sawa na asilimia 26.