TIMU YA RAINER ZIETLOW WAKARIBIA KUVUNJA REKODI YA DUNIA

Dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlow (katikati) akizungumza na wanahabari kuhusiana na rekodi yake ya kusafiri umbali mrefu Duniani mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwenye Ofisi za Alliance Autos, Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh na kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.
Na Mwandishi Wetu
DEREVA raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile za awali alizovunja mwaka 2011 na 2012.
Awali alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana kama `Panamerica’ambayo ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17 wakati ile ya `Russtralia’ ilimtoa Melbourne, Australia hadi St.Petersburg nchini Urusi ambako alitumia saa 18.
Zietlof anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI alianza rasmi safari yake Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway na anatarajia kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa kilometa 17,000.
Kwa mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu imempitisha katika nchi za Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Slovakia, Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya na sasa Tanzania.
Dereva huyo alizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya CFAO Motors yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa atachangia kiasi cha senti 20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji vya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (SOS) nchini Tanzania na Zambia.
Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.
Aidha, amelisifia gari hilo kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mazingira tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto pamoja na barabara mbovu.
Mradi huu wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa gari hilo umedhaminiwa na makampuni ya Tehama, magari ya Volkswagen ya Ujerumani, Slovakia na Afrika Kusini.
Katika safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake wawili, Marius Biela ambaye ni mpiga picha na mchukua video; Matthias Prillwitz ambaye ni mzoefu wa mbio za magari nchini Ujerumani.
Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na ameoa na ana mtoto mmoja.
Dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof (wa kwanza kulia )akiwaelezea jambo wanahabari hawapo pichani Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Ltd. Tharaia Ahmed
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akielezea ni kwa namna gani magari yao yako imara kuhimili masafa marefu akitolea mfano gari ya Volkswagen aliyosafiri nayo dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof.
Dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akioyesha cheti cha rekodi ya dunia mbele ya wanahabari
Dereva toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Dereva toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya injini ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi zaidi ya 19 Duniani.
Dereva toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya bodi ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi zaidi ya 19 Duniani.
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya sehemu ya kuweka vifaa vya akiba kwenye gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiendelea kutoa maelekezo ya Gari yake hiyo aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Gari aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI inavyoonekana kwa ndani.
12
Dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (wa pili toka kulia) wakipata picha ya pamoja na wanahabari.
15
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (kushoto) akipata picha na Dereva toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof
Meneja Masoko wa CFAO Motors Ltd. Tharaia Ahmed(kushoto) akipata picha na Dereva Rainer Zietlof.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akisoma cheti cha rekodi ya dunia alichopewa dereva toka Ujerumani.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post