Katibu
mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)
Taifa Ndugu Sixtus Mapunda amepata makubwa wilayani Mbinga yaliyoacha
gumzo kubwa wilayani hapo. Mapunda ambaye alitoke wilaya ya Nyasa
amepokelewa kwa kishindo kikubwa na viongozi wa CCM pamoja na mamia
ya wananchi wa wilaya ya Mbinga ambako ndipo alikozaliwa.
Mapunda
ameingia Mbinga jana akitokea wilaya ya Nyasa ambapo ni muendelezo wa
ziara yake ya siku tano (5) Mkoani Ruvuma. Ziara ambayo inalenga
kukagua na kuhamasisha ujenzi na uimara wa jumuiya mkoani humo pamoja
na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha mapinduzi ya mwaka
2010-2015.
Katika hotuba yake
Katibu Mkuu amewataka wananchi wa Mbinga kujitokeza kwa wingi na
kuwachagua wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi katika
uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotegemewa kufanyika mapema mwezi
ujao pamoja na uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2015.
Pia Katibu Mkuu,
Mapunda amemtembelea Mzee Constantine O. Millinga mmoja wa waasisi
kumi na watano (15) walioanzisha Chama Cha Ukombozi cha TANU
wakiongozwa na Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, mnamo tarehe 7.7 1954. Mzee Millinga ni miongoni mwa wawili
kati ya waasisi hao ambao wako hai mpaka hivi sasa.
Mapunda ametoa wito
kwaWatanzania, wananchama wa Chama Cha Mapinduzi na hasa Vijana wa
Taifa hili, kuwaenzi na kuwatembelea wazee ambao ni waasisi,
wazalendo wa kweli na wapigania uhuru wa nchi hii, ambao wametuwekea
misingi ya Umoja na Utaifa ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya
amani na utulivu.
Katibu Mkuu huyo wa
UVCCM anaendelea na ziara yake Mkoani Ruvuma ambapo atatembelea
wilaya ya Namtumbo na baadae Songea Mjini ambako atahutubia mkutano
mkubwa wa hadhara katika wilaya hiyo ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa
Ruvuma.
|