mtuhumiwa
Hamis Mohamed (47) Mkazi wa Kondoa aliyekamatwa eneo la Mianzini jijini
Arusha akiwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi iliyokuwa
inasafirishwa toka nchi jirani ya Kenya kuelekea Kondoa mkoani Dodoma
Mtu mmoja aitwaye
Hamis Mohamed (47) Mkazi wa Kondoa mkoa wa Dodoma, amekamatwa na Jeshi la
Polisi Mkoa wa Arusha baada ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi
aliyekuwa anaisafirisha kwa mtindo wa aina yake.
Akiongea na
waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba tukio hilo
lilitokea tarehe 05.11.2014 muda wa saa 11:00 jioni eneo la Mianzini ambapo
mtuhumiwa huyo alikuwa anasafirisha madawa hayo kwenye gari aina ya Fusso basi
lenye namba za usajili T. 577 BFM ambapo aliihifadhi kwenye magunia mawili huku
juu na pembeni ya magunia hayo akiweka viatu.
‘’Katika magunia
yale alikuwa ameweka viatu na katikati aliweka viroba 36 vya madawa hayo aina
ya mirungi ambayo alikuwa anasafirisha toka nchini Kenya kupeleka Kondoa mkoani
Dodoma hivyo ukiangalia unaweza kusema ni viatu pekee’’. Alifafanua Kamanda
Sabas.
Alisema tukio hilo
lilifanikiwa kutokana na mahusiano mema yaliyopo kati ya Jeshi hilo na raia
wema ambao walitoa taarifa iliyofanyiwa kazi haraka na asakari wa Jeshi hilo.
Baada ya askari hao kupata taarifa hiyo
walianza kulifuatilia gari hilo na lilipofika maeneo ya Mianzini jijini hapa
kwenye maegesho ya basi hilo ndipo walipoanza kufanya upekuzi na kufanikiwa
kukamata magunia hayo yaliyokuwa na viatu vilivyochanganywa na madawa hayo.
Kamanda Sabas
alisema kwamba mtuhumiwa huyo bado anaendelea kuhojiwa na atafikishwa
mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia