Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando akifungua kongamano hilo la kisayansi.
Na Andrew Chale, Bagamoyo
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepongeza juhudi za makusudi zinazofanywa na Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) katika kushughulikia masuala ya afya kwa jamii huku ikiahidi kushirkiana kwa ukaribu.
Hayo yalisemwa jana mjini hapa na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk.Donan Mmbando wakati wa ufunguzi wa kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA unaoendelea katika ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo.
Dk.Margaret Mmbando alisema kuwa juhudi za dhati zinazofanywa na wadau wa afya serikali inazitambua na watahakikisha wanaendelea kuungana nao kwa hali na mali ilikuisaidia jamaii kwenye mambo yote ya msingi hususani masuala ya afya.
"Tunaipongeza TPHA kwa juhudi hizi za dhati kabisa katka ukuaji na ustawi wa sekta ya afya. Hivyo pia naamini baada ya kongamano hili kwa muda wa siku tano kila atakayetoka hapa atajifunza mambo makubwa na ya msingi katika mustakaba wa sekta hii" alisema Dk.Margaret Mhando.
Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga (kulia) akimkaribisha, Dk. Margaret Mhando kwenye ufunguzi huo.
Aidha aliwataka TPHA kutanuka zaidi kuwa na matawi mengi ikiwemo kufika pembezoni mwa nchini ilikuweza kutanua huduma zao hizo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe alisema kongamano hilo la kisayansi la 31, linatarajia kuwa la siku tano na kutarajia kumalizika Novemba 28 ambapo wataalamu wa afya na wadau watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.
Naye Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga alisema kongamano hilo ni la kuwakutanisha wataalamu ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na kutoa mapendekezo namna ya kuleta mabadiliko katika jamii.
“Kongamano la kisayansi na mkutano mkuu wa mwaka unahusisha wataalamu wa kisayansi wa ndani na nje ya Tanzania ambapo watajadili masuala ya jamii na maendeleo ya milenia,” alisema Dk. Kisanga na kubainisha kwamba shughuli hiyo itahitimishwa Novemba 28.
Mkutano huo leo unaingia siku ya pili ambapo wajumbe wa TPHA, wanachama na wadau wa sekt za afya na mambo ya jamii wameendelea kujadili mambo mbalimbali katika ukuaji wa sekta ya afya hapa nchini.
Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk. Elihuruma Nangawe akitoa lecture katika kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wakifuatlia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mgeni rasmi Dk. Margaret Mhando kwenye picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua kongamano hilo.