Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee akifungua rasmi warsha ya siku moja ya iliyohusisha wadau mbalimbali wa maendeleo, kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs), iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF) iliyofanyika hivi karibuni visiwani Zanzibar. Kulia kwake ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.
Na mwandishi wetu, Zanzibar
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Zanzibar katika kuangalia masuala muhimu yanayohusu muktadha ujao wa kufanikisha uondoaji wa umaskini uliotopea (SDGs) baada ya kukamilika kwa programu ya maendeleo ya milenia (MDGS).
Alisema kitendo cha serikali kuandaa warsha ya kupashana kuhusu programu hiyo mpya kabla ya mazungumzo na mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo ni washirika wa maendeleo kuhusu SDGs kunaonesha dhamira ya dhati kwa serikali kuendelea kusukuma mbele maendeleo yenye lengo la kunemeesha wananchi.
Mratibu huyo alisema hayo hivi karibuni katika warsha iliyofungulia na Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee iliyokusanya wadau mbalimbali wa maendeleo kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs),iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF).
Warsha hiyo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Programu wa ESRF Dk. Tausi Kida warsha hiyo ni sehemu ya kuelezana kuhusu mkakati huo mpya wa Umoja wa Mataifa unachukua nafasi ya MDGs na nafasi ya Tanzania katika kutekeleza malengo hayo ya kimataifa.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo kwenye warsha ya siku moja ya kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs), iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF) iliyofanyika hivi karibuni visiwani Zanzibar. Kushoto kwake ni mgeni rasmi Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee, Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Amina Khamis Shaaban na Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida.
Warsha hiyo imefadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNDP, UNAIDS na UNWOMEN.
Mratibu huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa amesema kwamba agenda zilizopangwa kujadiliwa zinaonesha ujasiri wa Tanzania katika kuhakikisha inashiriki kwenye ajenda za dunia kwa kutekeleza nafasi yake katika mipango ya maendeleo na ustawi wa jamii kwa kuzingatia usawa wa jinsia.
Alisema shughuli inayofanywa sasa ya kuwasilisha malengo hayo kwa majadiliano miongoni mwa wadau mbalimbali kabla ya majadiliano rasmi kati ya mashirika ya Umoja wa mataifa na serikali ni ya maana katika kuongeza uelewa na kuimarishwa kwa mawazo muhimu.
Warsha ya kwanza ya aina hiyo ilifanyika Oktoba 27 jijini Dar es Salaam ambapo wadau mbalimbali wakiwemo wanazuoni, wawakilishi wa serikali, taasisi zisizo za kiserikali na wengineo walijadiliana kuhusu SDGs na kama malengo yake yanawezwa kutekelezwa.
Aidha warsha hiyo ilijadili kama malengo hayo yanawezwa kutumiwa na watunga sera na kuleta tofauti inayotakiwa na kama malengo hayo yanahitaji kuboreshwa zaidi ili kujua kitu cha kufanya na kama umma unaweza kujipanga kutekeleza malengo hayo.
Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi gani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.
Alvaro alisema agenda hizo zinakwenda vyema na mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa kwa Tanzania (UNDAP) kwa kuwa imejikita katika maeneo muhimu yanayopambana na kutokomeza umaskini na kuwa na maendeleo endelevu.
Maeneo hayo ni pamoja na malengo ya milenia ambayo hayajatekelezwa kwa ukamilifu, nishati, mabadiliko ya tabia nchi,mazingira na kujenga jamii yenye amani na kujali maendeleo.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Zanzibar Beach resort, Katibu Mkuu alisema ni vyema wazanzibari wakatumia nafasi hiyo kutengeneza mkakati wa Zanzibar wanayoitaka, Zanzibar yenye maendeleo inayojali haki na yenye amani.
Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini zinazoendelea.
Aliwataka wana warsha kutumia nafasi hiyo kujipanga vilivyo katika kuhakikisha wanajua kinachotokea duniani katika sekta ya maendeleo na kutumia nafasi hiyo kutengeneza muskabali wa wazanzibari unaoendana na malengo ya dunia ya kutokomeza umaskini na kujenga nchi yenye kujali maslahi ya jamii yenye maendeleo endelevu na amani.
Alisema mafanikio ya malengo ya milenia yaliyojikita katika kutokomeza umaskini na njaa, kufanikisha elimu ya msingi kuyaleta usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na kupunguza vifo vya watoto na wanawake wajawazito, kukabiliana na Ukimwi, kuhakikisha mazingira endelevu na kuleta mshikamano wa kimataifa katika maendeleo yanatakiw akuendelezwa.
Alisema kwa miaka 15 zanzibar imefanya vyema katika programu hizo na kutaka wadau kufikiria kuimarisha na kuangalia kwenye udhaifu ili kuyakamilisha kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mhadhiri wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
Pichani juu na chini ni wadau mbalimbali wa maendeleo waliohudhuria warsha hiyo ya siku moja ya kujadili na kuangalia malengo ya programu ya maendeleo endelevu (SDGs), iliyoandaliwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF) na kufadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNDP, UNAIDS na UNWOMEN.
Pichani juu na chini ni washiriki wa warsha hiyo ya siku moja wakichangia hoja wakati wa majadiliano.
Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na washiriki wa warsha hiyo.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Mzee(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.