WAFUGAJI WAVAMIA ENEO LA MWEKEZAJI,WACHOMA MOTO NYUMBA NA MAGARI.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Siha ,Rashid Kitambulilo akimuongoza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakati akitembelea eneo la mwekezaji la Tanganyika Film and Safari ambako wafugaji jamii ya Masai wanadaiwa kufanya uharibifu mkubwa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakitizama uharibifu  uliofanywa na wafugaji jamii ya Masai.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akitizama moja ya gari lililochomwa moto na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji jamii ya Masai.
Askari Polisi walilazmika kuongeza ulinzi katika eneo hilo.
Mkuu wa mkoa ,Gama akiteta jambo na baadhi ya viongozi ambao ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama.



Vikao vikiendelea eneo la mwekezaji.

Uharibifu mkubwa umefanyika ambapo nyumba 16 na magari tisa yameteketea moto.
Mwekezaji Peter Jones akizungumza na wanahabari kuhusu tukio hilo lililomsababishia hasara kubwa.
Vikosi vya askari Polisi kutoka Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro vililazimika kupiga kambi kwa muda katika eneo hilo ili kuwadhibiti wafugaji hao

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post