Mwanamke
mmoja mkazi wa kijiji cha Olkokola Wilayani Arumeru Mkoani Arusha
amefanyiwa ukatili wa kutisha kwa kukatwakatwa na Panga kichwani na
kuondolewa kiganja cha Mkono, sikio na sehemu nyingine za mwili wake .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP, Liberatus Sabas
Mwanamke
mmoja mkazi wa kijiji cha Olkokola Wilayani Arumeru Mkoani Arusha
amefanyiwa ukatili wa kutisha kwa kukatwakatwa na Panga kichwani na
kuondolewa kiganja cha Mkono, sikio na sehemu nyingine za mwili wake
Mwanamke
huyo anayefahamika kwa jina la Paulina Joseph amefanyiwa ukatili huo na
mtu anayedaiwa kuwa ni shemeji yake kwa madai ya kuingilia ndoa yake.
Tukio hilo lilimkuta bi Paulina akiwa shambani kwake akikata nyasi kwa ajili ya kulisha mifugo.
Mume wa
Paulina ameeleza masikitiko yake kwa uongozi wa kijiji,Kitongoji na kata
kwa kushindwa kumkamata mtuhumiwa na kutoroka kwani kitendo hicho
kinaweza kusababisha kuendelea kwa vitendo vya ukatii dhidi ta wanawake
nchini.
Viongozi
wa kijiji hicho wamekanusha kuwa hakuna uzembe uliofanyika kumkamata
mtuhumiwa huyo kwani bado inaendelea kumtafuta na kumtia hatiani.
Bi
Paulina anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospital Teule ya Seriani
wilayani Arumeru alipolazwa na hali yake bado sio nzuri.