Jumla ya kiasi cha $ 1 milioni
sawa na sh,1.6 bilioni kimetolewa kwa wajasiriamali mbalimbali hapa nchini kwa
lengo la kuwapatia mashine mbalimbali za kutengeneza bidhaa kama mkopo wa
masharti nafuu ili waweze kujikwamua katika biashara zao mbalimbali.
Kiasi hicho cha fedha kimetolewa na
shirika lililojikita kuwakopesha wajasiriamali wadogo wadogo mashine hizo la
Equity For Tanzania(EFTA) katika mikoa ya
Arusha,Mwanza,Kilimanjaro,Geita,Shinyanga,Simiyu,Mara na Manyara katika kipindi
cha mwaka 2004 hadi 2014.
Akizungumza na wakati akifunga
Maonyesho ya wajasiriamali waliowezeshwa na EFTA mkuu wa chuo cha Ufundi Arusha
DktarIRichard Massika alisema kuwa dhana ya kuwakopesha wajasiriamali mikopo ya Mashine
ni dhana nzuri kuliko kutoa pesa ambazo mara nyingi huelekea kwenye shughuli
zingine ambazo hazikuwa kwenye lengo lililokusudiwa.
Dkta Masika akwataka wajasiriamali
waliokopeshwa kuwa mabalozi wazuri wa marejesho ya mikopo ili shirika hilo
liweze kutoa mikopo kwa wajasiriamali wengi Zaidi na kujikuta watanzania
tunapunguza wimbi la vijana kukosa ajira.
“Tufike mahali tukawa wazalendo wa
kuwa mabalozi wazuri wa marejesho ya mikopo ili nkuweza kupunguza wimbi la
vijana kukosa ajira na shirika lenu lifike mbali Zaidi kwani kuna vijana wenye
nia ya kupata nafasi za mikopo ya mashine na teyari wameshaanza shughuli hivyo
mufikie hata hao kokote hapa nchini”alisema dkta Masika.
Alisema
kuwa watanzania wengi bado wanauhitaji wa kupata mikopo ya kijiinua
kiuchumi bila ya kuwaangalia hawa itafika mahali watakosa sehemu ya
kuweza kjiinua hivyo kukosa fursa endelevu ambazo zitaweza kuwajengea
kipato chao na kukuza uchumi wa taifa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi kabla ya kufunga
Maonyesho ya bidhaa zinazotengezwa na shirika hilo,meneja masoko wa shirika
hilo,Peter Temu alisema kuwa mikopo hiyo yenye masharti nafuu imetolewa kwa
lengo la kuwakwamua wajasiriamali hao ili waweze kupiga hatua katika biashara
zao.
Temu,alisema kuwa changamoto kuu
ambayo wamekuwa wakikumbana nayo katika majukumu yao ni pamoja na baadhi ya
wateja wao kutorudisha mikopo hiyo kwa wakati hali ambayo imekuwa ikiwakwanza
katika kutekeleza majukumu yao.
Awali meneja wa oparesheni na mipango
wa shirika hilo,Tim Ellis alisema kuwa mkakati wao hapo baadaye ni kupanua
huduma yao katika mikoa minane zaidi na kuwafikia watanzania wengi hususani
walio katika maeneo ya vijijini .
Alisema kwamba wamekuwa
wakishirikiana na wafadhili mbalimbali katika majukumu yao huku akiwataja
baadhi yao kuwa ni pamoja na benki ya dunia(WB),Africa Enterprise Challenge
Fund(AECF) pamoja na wawekezaji binafsi walioko hapa nchini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia