Simanzi
zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 10 kufariki dunia
katika ajali
iliyotokea eneo la Tengeru. Akiongea na mwandishi wetu mmoja ya
mashuhuda aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema
ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadc-Kwa Fundi
iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka
Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.Aliongeza kuwa chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la abiria)
iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso kwa uso na
lori hilo. Habari kamili zitawajia punde.