Pichani juu na chini ni baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na watoto wa wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walipojumuika pamoja mwishoni mwa juma kushiriki michezo mbalimbali kwenye UN Family Day kusheherekea maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanishwa kwake.
Watoto wakifurahia kupakwa rangi usoni katika bonanza la UN Family Day ikiwa ni shamra shamra ya maadhimisho ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Wow...... watoto wakionyesha michoro yao kwa mpiga picha kwenye bonanza la UN Family Day.
Timu ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa (jezi za blue bahari) na timu ya wafanyakazi wa Wizaya ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimenyana uwanjani kwenye UN Family Day iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya michezo Gymkhana ambapo timu ya Umoja wa Mataifa iliibuka kidedea kwa kuinyika timu ya Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bao 3-0.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakishangilia ushindi baada ya kuibuka kidedea kwenye mechi ya kirafiki na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa katika kwenye bonanza la UN Family Day lililofanyika mwishoni mwa juma.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) Bw. Philippe Poinsot nao walijumuika na wafanyakazi wenzao katika UN Family Day kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem (mwenye t-shirt nyeupe) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye bonanza la UN Family Day wakijiandaa na zoezi la kukabidhi medali kwa timu zilizocheza mechi ya kirafiki.
Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem, Mwakilishi Mkazi wa FAO, Diana Templeman, Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania, Dk Rufaro Chatora na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakipata picha ya pamoja kabla ya kukabidhi zawadi kwa timu zilizomenyana kwenye bonanza la UN Family Day.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwavisha medali timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyonyukwa bao 3-0 .Kulia ni Sawiche Wamunza kutoka UNFPA.
Kapteni wa timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kukabidhiwa kikombe.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akikabidhi kikombe kwa Kapteni wa timu ya Umoja wa Mataifa Laurean Kiiza iliyoibuka kidedea kwenye mechi ya kirafiki bonanza la UN Family Day.
Kapteni wa timu ya Umoja wa Mataifa Laurean Kiiza akifurahia kikombe walichokabidhiwa baada ya kuitandika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bao 3-0.
Tatu bila tatu bila.......Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania, Dk Rufaro Chatora akijumuika na timu ya Umoja wa mataifa kushangilia ushindi huo huku wakiimba.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) akifurahi jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) pamoja na Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania, Dk Rufaro Chatora kwenye bonanza la UN Family Day ikiwa ni shamra shamra ya maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akibadilishana mawazo na Naibu Mkurugenzi Mkazi, Oparesheni wa UNDP, Bw. Titus Osundina.
UN Care waliweka mabanda kwa ajili ya kutoa elimu ya afya ikiwemo ya Uzazi wa mpango, Ugonjwa Ebola, Upimaji wa VVU na ushauri nasaha, kansa ya matiti na mengine mengi kwenye bonanza la UN Family Day lililofanyika mwishoni mwa juma.
Watoa huduma za afya wakifanya kipimo kwa mmoja wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliohudhuria bonanza la UN Family Day kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Mtoa ushauri nasaha na upimaji wa VVU kutoka Angaza (kushoto) akimsikiliza na mmoja wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kabla ya kumfanyia vipimo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika banda lake la kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola
Muonekano wa moja ya mabanda ya kutoa elimu ya afya katika bonanza la UN Family Day.
Petra Karamagi wa ofisi za Mratibu Mkazi akibadilishana mawazo na MC wa UN Family Day, Usia Nkhoma Ledama kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar.
Maakuli yalihusika pia....kazi na dawa..!
Kwa picha zaidi ingia hapa
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia