Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Bernard Membe
Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa wakati
alipowasili katika Kiwalala Kituo cha Ufugaji cha Masister cha Narunyu
ambapo ameshiriki kazi ya kukamua maziwa akiwa katika ziara yake ya
kikazi ya mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali lakini pia
kuhimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi CCM, Katibu mkuu Kinana katika
ziara hiyo anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na
Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
kazi ya kukamua maziwa katika kituo cha uugaji cha Masister cha Narunyu
Mtama mkoani Lindi wakati alipotembelea kituo hicho.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya Masister mara baada ya kuwasili katika kituo hicho katika jimbo la Mtama mkoani Lindi.
Baadhi ya Ng'ombe wakiwa katika shamba hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa tanki la maji katika mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Nyangamara jimbo la Mtama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa tanki la maji katika mradi wa maji unaojengwa katika kata ya Nyangamara jimbo la Mtama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha
kitabu kinachoelezea shughuli mbalimbali zilizotekelezwa na Mbunge wa
jimbo la Mtama Mh. Bernard Membe alipotembelea ofisi ya mbunge huyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
katika shughuli za kubangua korosho wakati alipotembelea kikundi cha
akina mama cha kubangua korosho katika kata ya Nyegendi jimbo la Mtama.