MOTO MKUBWA WATETEZA SOKO LA BIDHAA ZA UTAMADUNI LIJULIKANALO KAMA MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET
















SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET limetea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo



Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.



Mulongo ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto na kusababisha hasara kwa wananchi.



"Sitakubali kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi za Chama Cha mapinduzi wilaya yalipo maduka haya"amesema Mulongo



Chanzo cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao.
Habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post