kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Lineratus Sabas aakionyesho moja ya silaha ambazo zimesalimishwa na wananchi
Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG ambazo zilisalimishwa na wananchi katika mbili
tofauti huko wilayani ngorongoro.
Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani
Arusha Lineratus Sabas alisema kuwa
Silaha hizo zilisalimishwa na wananchi katika siku tofa uti tofauti ambapo
alisema kuwa silaha ya kwanza ilisalimishwa September 19 silaha aina ya SMG yenye
NO.563651071iliopatikana katika eneo la harash ikiwa na risasi mbili ndani ya magazine .
Alibainisha kuwa silaha ingine ilisalimishwa September 26 ikiwa ni aina ya SMG yenye namba ya usajili 514142 hii ilipatika katika
eneo ilo ilo la la harash wilayani Ngorongoro
Aliwapongeza wanachi kwa kutii sheria ya kusalimisha silaha
hiiuku akitoa wito kwa wananachi wote popote pale walipo kusalimisha silaha
ambazo wanahisi wanazitumia kinyume cha sheria.
Aidha alisema kuwa kama kuna mwananchi yeyote anaisi kuwa
anamali nyingi na anaitaji kumiliki silaha basi afuate sheria zinazotakiwa .
habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog