baadhi ya wananchama wapya wa ccm wakiwa wanapunga mara baada kukaribishwa katika chama
Wanachama
wa CCM na viongozi wao mjini Moshi walifanya mkutano wa hadhara katika
maeneo ya Pasua,Moshi mjini siku ya jumamosi 18 April 2015,
katika
mkutano huo ulioudhuriwa na mamia ya watu uliweza kuvuta hisia za wengi
na katika waliovutika ni pamoja na wanachama 24 wa CHADEMA ambao
walirudisha kadi za Chadema na kujiunga na CCM.
Jimbo
la mjini Moshi limekuwa gumozo la kiasa kabla ya uchaguzi mkuu kutoaka
na baadhi ya wananchi na vikundi mbali mbali vya kijamii kujitokeza kwa
kumshawishi kijana moja ajulikanae kwa jina la Daudi Babu Mrindoko
achukue fomu za kugombea ubunge 2015,kitendo hiko cha kumshawishi kijana
huyo ,kimekuwa kama cheche za moto zilinazosemekena kuwa baadhi ya
vigogo kujitangaza kutogombe tena nafasi zao za udiwani na ubunge.
Baadhi
ya wakazi wa Moshi wanadai kuwa wanataka mabadiriko 2015 wapate mbunge
kijana mwenye uwezo na wepesi wa kuwatumikia,ambaye atakuwa kiungo wa
jamii yote ya wakazi wa Moshi,wanajaribu kushawishi kijana
Daudi Mrindoko lakini mwenyewe bado yupo kimya ! wenyewe wanamwita Obama
wa Moshi mjini.