Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Kushoto) na Kaimu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia)
wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Kunduchi Beach jijini
Dar es salaam kwa ajili ya kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa
wizara ya nishati na madini unaoanza tarehe 01 hadi tarehe 02, Aprili
2015 wenye lengo la kujadili mafanikio na changamoto katika utendaji
kazi wa Wizara pamoja na taasisi zake.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE) Wizara ya
Nishati na Madini, Marcelina Mshumbusi akisoma hotuba ya kumkaribisha
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava
(hayupo pichani) katika mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa TUGHE Wizara
ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini
wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Charles Kitwanga (hayupo pichani).
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava
(kulia) akisoma hotuba ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Charles Kitwanga (wa kwanza kushoto). Katikati ni Katibu wa
TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
Sekretarieti
inayoratibu mkutano wa baraza la wafanyakazi la Wizara ya Nishati
na Madini wakisikiliza kwa makini na kunukuu mada zilizokuwa
zinawasilishwa katika mkutano huo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini.
Baadhi
ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini
wakiimba wimbo wa kuonyesha mshikamano ujulikanao kwa jina la
“solidarity forever”.
Baadhi
ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi kutoka Wizara ya Nishati na
Madini wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa katika mkutano huo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na
Mhasibu Mkuu Mfawidhi wa Wizara ya Nishati na Madini, Michael Marandu
(kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano ili kufungua
mkutano huo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga (katikati, waliokaa
mbele) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi, Wizara
ya Nishati na Madini.