picha maktaba
Na Woinde shizza wa libeneke la kaskazini blog
Na Woinde shizza wa libeneke la kaskazini blog
Wakandarasi nchini wametakiwa kuzingatia ubora ,viwango vya kazi zao ili kuweza kutekeleza kazi zao
kwa ufanisi zaidi na kuweza kufanya bkazi yenye viwango vya hali ya juu pindi
wanapo tekeleza miradi mbalimbali nchini.
Endapo wakandarasi wazawa wataweza kuzingatia taratibu za
viwango vya ujenzi pindio wanapopata
zabuni za miradi ya ujenzi hali hiyo itaongeza chachu ya mabadiliko na kuweza
kushasishi serikali kuyweza kuwa wanawatumia wakandarasi wazawa ili kuepuka
gharama za kutoa zabuni kwa wakandarasi wageni
ili kuweza kutumia ghara ma ndogo na pesa ziweze kubaki nchini na kutopelekwa kwa nchi
za wakandarasi wageni.
Hayo yameelezwa leo na Mhandisi Omari Kiure
kutoka kampuni ya Kiure Engineering Limited kutoka mkoani hapa wakati akiongea na waandishi wa habari mara
baada ya kukabidhi jengo la kituo cha
jimolojia Tanzania ambapio kituo hicho kiko chini ya Wizara ya nishati na madini ambacho kimejengwa
eneo la njiro mkoani Arusha.
Hata hivyo jengo hilo limegharimu zaidi ya shilingi bilioni
moja ambalo nikituo cha kutoa mafunzo kwa wanafunzi namna ya kuongeza thamani
madini ya vito,mafunzo ya ukataji madini
,utengenmezaji bizaa za mapambo sambamba na uchongaji vinyago vya mawe ili
kuweza kuongeza ajira kwa vijana walio wengi ambalo ndilo kundi kubwa nchini
ambalo halina ajira.
Aidha aliongeza kuwa
endapo wkandarasi watajizatiti na
kuboresha kazi zao wataweza kufanya
kazi ambazo zinzonekana katika viwango
vya hali ya juu ili kuwezaa kushawishi wadau mbalimbali kuweza kuwapa miradi ya
ujenzi pindi inapohitajika na kuweza kutokuwepo dosari ama kuanguka kwa
magorofa baada ya muda mchache hali inayogharimu Serikali fedha nyingi ambazo
bni kodi za wananchi.
Kwa upande wake mhitimu wea kituo hicho Bi,Salome Mollel alisema kuwa
ujenzi wa kituo hicho kitakuwa mkombazi wa vijana kupata mafunzo hayo na
kuweza kupata ajira kwa wafanyabiashara wa mawe
kwani kulikuwa na changamoto kubwa sana ya kituo cha mafunzo ya
uongezaji thamani ya vito vya madini hali iliyokuwa inawalazimu wafanyabiahsra
hao kuuza madini yakiwa ghafi nsa kuuza kwa bei ya hasara na fedha nyingi kuenda nchi nyingine.
Ambapo kupitia kituo hicho kitawasaidia vijana kupata ajira
na kuongeza thamani ya madini hayo na itawawezewsha wafanyabiahsra hao kuuza
madini yakiwa yameongezwa thamani ili kupata bei nzuri na fedha kubaki na
kuomgeza uchumi wan chi.