Ilikua
mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa
harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija
cha
kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za
furaha
za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati
hao
ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni
kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu
wa ngozi.
|
Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji
ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni
hapo. |
|
Huyu ni Irene wa NHIF
Shinyanga |
|
Wajumbe wa Imetosha |
Akiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za
Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa
haki ya kuishi kwa
kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji
na
unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi. "Tunatambua hapa
kati yenu kuna vipaji vya aina
mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza
mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo
mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau" alisema
Masoud.
|
Kipanya akimuimbisha mtoto wa kituoni
hapo |
|
Mwl Peter Alali Francis akisisitiza jambo
wakati akiongea na ujumbe wa Imetosha |
Alisema"Pamoja na uhaba wa mabweni kituo kinakabiliwa na
uhaba
wa chakula. Muda mwingine watoto hawa hushindia mlo mmoja. Chakula
mlichofikisha leo hapa kitatusogeza maana tulikua tumeishiwa chakula
kabisa"
alisema Francis. Ujumbe huo wa Imetosha uliwasilisha kambini hapo unga
kilo 50, mchele kilo 50, chumvi kilo 5 na mafuta ya kupikia lita
10.
Mwalimu
Mkuu wa Kituo hicho Peter Ajali Francis
alishukuru ujio wa wanaharakati wa Imetosha kituoni hapo na kusema kituo
hicho
kilianzishwa mwaka 1960 kikiwa chini ya Kanisa
katoliki.
Kituo
hicho kilikua maalumu kwa ajli ya watoto wasiiona na viziwi lakini kutokana
na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
kuongezeka mwaka 2006 kituo hicho kilianza kupokea watoto wenye
ulemavu wa
ngozi kutoka sehemu mbalimbali toka kanda ya Ziwa. Kituo kina jumla ya
watoto 388 kati ta hao 284
wana ulemavu wa ngozi. Kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa mabweni
ambapo
chumba chenye uwezo wa kuchukua watoto 50 kinachukua watoto zaidi ya
100 na chenye uwezo wa
kuchukua watoto 40 kinachukua watoto zaidi ya
80.
Zaytun Biboze akiwa amebeba mmoja
wa watototo wanaoishi katika ktuo hicho
|
Masoud Kipanya na Jhikoman wakiwaimbisha
watototo wimbo waupenda wa Clap your hands! |
|
Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga akiwachekesha
watoto kiuoni Buhangija, Shinyanga |
|
Magunia haya ya unga, mafuta na mchele ndio
msaada wa chakula ambao Imetosha ilitoa kwa kituo hicho |
|
Katibu wa Imetosha amabaye ki taaluma ni
mwandishi wa habari akimhoji mwalimu Francis Ajali |
Wanaharakati wa Imetosha wamepanga kurudi tena mjini Shinyanga mwezi
Mei na kukifanya kituo hicho kuwa ngome ya kuanzishia mapambano dhidi ya
unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa albino.
Picha na Mkala
Fundikira habari na Salome Gregoy/ Mkala Fundikira