PICHA na maktaba kikosi cha jkt oljoro |
Timu ya maafande wa Jkt Oljoro yenye makazi yake jijini Arusha
imepania haswa kupanda ligi kuu msimu wa ligi unaofuata baada ya
wachezaji wake kuingia kambini mapema wiki hii kwa mazoezi mepesi
wakimsubiria kwa hamu kubwa kocha wao Mbwana Makata huku wakijitamba
hakuna machawi tena wa kuwabakiza ligi daraja la kwanza.
Wachezaji
hao wanaoonekana katika milima na uwanja wa chuo cha uhasibu ulioko nje
kidogo ya mji wameonekana kujifua kwa kasi kwa mbio mbali mbali
sambamba na mazoezi ya hapa pale kujiandaa ya michuano ya ligi daraja la
kwanza mwezi Agost huku wakijisemea “kwa mwaka huu hakuna mchawi kutoka
duniani atakaeweza kuwazuia kupanda ligi kuu”
Katibu
mkuu wa timu hiyo, Hussein Nalinga alisema kuwa hadi sasa wachezaji 15
wamerejea kambini ambapo hadi ijumaa hii wachezaji wote wataingia
kambini na kufikisha idadi ya 28 ambao watajiunga na kocha mkuu baadae
M’bwana Makata baada ya msimu wa ligi kuu kwisha ambapo kwa Prison
imebakiza mechi tatu.
“Timu
kwa sasa inarejea kambini ambapo wamefikia wachezaji 15 na wengine 13
wanaingia kesho hadi ijumaa na wanafundishwa na kocha msaidizi Sande
Mussa hadi pale kocha wetu anaefundisha Timu ya Prison kurejea katika
clabu yetu”
“Mimi
niseme tu kwa mwaka huu Mungu yupo nasi na hakuna wa kutuzuia kupanda
ligi kuu si timu zilizoko wala uwezo wa wachezaji wetu, ndio maana
tunaanza mazoezi mapemaa ili kujifua ipasavyo ukiachilia mbali usajili
wa kufa tutakaofanya msimu huu hivyo wana Arusha watoe sapoti yao kubwa
kwa timu hasa ushauri kwani tunakata kiu yao ya kukosa ligi kuu msimu
ukianza”