Wanachama na
mashabiki wa chama cha Mapinduzi wametakiwa kujipanga kuhakikisha jimbo
linarudi mikononi mwao kutoka kwa wapangaji ambao kodi yao imeisha chama cha
demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kwenye uchaguzi ujao ocktoba mwaka huu na kuwa
ushindi ni lazima kwa chama chao.
Kauli hiyo
imetolewa na kamanda wa vijana mkoani hapa Philemon Mollel wakati wakitoa neno la
shukrani kwenye chakula alichowaandalia wanachama na mashabiki wa CCM pamoja na
wananchi wa kata ya Unga ltd kwa ushindi walioupata kwenye uchaguzi wa serikali
za mitaa.
Mollel
aliwataka kuanza kujiandaa kuchukua jimbo hilo lililopo mikononi mwa Chadema
kwani ushindi wa chama hicho upo wazi na kuacha migawanyiko isiyo na lazima
ambayo iliwafanya kulikodisha jimbo hilo kwa mbunge wa sasa Godbless Lema.
Alisema kuwa
migogoro iliyokuwepo ndani ya chama hicho hapo kabla iliwafanya kutoa mwanya
kwa washindani kushinda na hivyo muda umefika wa kodi yao imemalizika sasa ni
zamu ya chama hicho kurudisha jimbo hilo.
“Hakika
natambua kuwa kila ukipanda mbegu nzuri utavuna mazao mazuri hivyo sisi
tuliwapangisha hatukuwajua walahatukutaka kuwajua vizuri sasa tumevuna
tulichakipanda kwa miaka mitano tusije tukajaribu tena kula sumu”alisema Mollel
Nae Diwani
wa kata ya Unga Ltd Issa Said Aliwataka wakazi wa kata hiyo wakati ukifika wa
kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kujitokeza kujiandikisha
na baadae kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura ya
maoni na kuwachagua viongozi.
Alisema kuwa
kumekuwepo na wananchi wanaoshindwa kuitumia nafasi yao ya kikatiba kuwachagua
viongozi na baadae wamekuwa wakitoa lawama kuwa wamechaguliwa viongozi wasiofaa
hivyo akawataka kujitokeza kumchagua kiongozi wanaemtaka kwa manufaa ya kata
yao na jimbo la Arusha na Tanzania kwa ujumla
“Kwanza
namshukuru muumba na pili namshukuru Kamanda kwa kutimiza ahadi aliyoweka
wakati wa kampeni kuwa atatoa Ng’ombe kwa kata itakayoshinda mitaa mingi na
sisi kuibuka kidedea kwa kushinda mitaa mitano kati ya sita iliyopo kwenye kata
hii”alisema Said
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Unga Ltd Sophia Munisi alisema kuwa
watahakikisha chama hicho kinapata ushindi katika uchaguzi uliopo mbele yao
tena wa kishindo kuhakikisha salamu ziawafikia wapangaji wote waliopangishwa na
chama hicho kwenye uchaguzi uliopita .
Munisi
alisema kuwa ifike mahali washindani wao wanadi sera na kuacha manung’uniko
yasio na lazima kwani chama kilichopo madarakani kimeendelea kuwaletea wananchi
maendeleo na kutekeleza ilani ya uchaguzi uliopita kwa asilimia kubwa hivyo
sasa ni wakati wa kukamilisha yale
yaliobakia .