Ticker

6/recent/ticker-posts

TANGAZO LA UANDIKISHWAJI WA WANANCHAMA WA TBN

Uandikishaji Wanachama 'Tanzania Bloggers Network' (TBN), 22/04/2015

Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania
Bloggers Network' - TBN

kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za
kujiunga zinatolewa. Wahusika

ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums)
Tanzania na Watanzania

wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.

Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu
ianze kuendeshwa

mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga
fomu hizo zinapatikana

kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar
Free Market lililopo

mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/-
ikiwa ni Kiingilio cha

mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa
mwanachama na shs 10,000/-

ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila
mwanachama anatakiwa

kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu
zitatolewa siku za kazi kuanzia

saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na
Mweka Hazina wa TBN,

Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media,
mjini Jengo refu karibu

na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili.

Kwa wanachama wa mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo
mara moja na wanachama

watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN. Utaratibu
unafanywa kupata viongozi wa

kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa kushirikiana na viongozi wa muda wa
TBN taifa. Viongozi wa

muda wa mikoa na kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu
zoezi la kujiunga

uwanachama wa TBN.

Mikoani TBN itagawanyika kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa
ya Tanga na Pwani

yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar es
salaam, Kanda ya Nyanda

za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda
ya Kusini (jumuisha

mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora,
Morogoro na Singida),

Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya Ziwa
(yenye mikoa ya Kagera,

Geita, Mara na Mwanza), na Kanda ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha na

Manyara).

Kwa wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama
wa TBN utafanyika kwa

muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili kutoa fursa kwa viongozi
na kamati husika

kutathmini wanachama waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi
sita.

NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini
coppy hiyo wataigharamia

wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa
mikoani kwa gharama za

TBN.

Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

Post a Comment

0 Comments