Na Woinde Shizza wa Libeneke la kaskazini blog
Jiji
la Arusha bado linakabiliwa na changamoto ua ugonjwa ambao unaambukizwa
kwa njia ya mkojo(U.T.I) ambao unakuwa siku hadi siku ambapo takwimu za
mwaka 2014 zinaonyesha kuwa takribani wagonjwa 32085 walikutwa na
ugonjwa huo hali ambayo inakwamisha jitihada za kujiletea maendeleo
kutokana na ugonjwa huo.
Ambapo
alisema kuwa hadi hivi sasa hawajagundua tatizo na chnanzo halisi cha
ugonjwa huo ambao unakuwa kwa kasi sana katika jiji hili la arusha hali
mabayo inakwamisha jitihada za kupambana na adui maradhi kwa wananchi
wake.
Hayo yameelezwa jana
na kaimu mganga mkuu wa jiji la Arusha Sr,Jane Balalukululiza wakati
akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake na kuweza kuelezea ugonjwa
huo amabo umekuwa ni tatizo lajiji kwa wananchi wake,mahojiano hayo
yaklifanyika ofisini kwake katika jiji hili mkoa wa Arusha.
Hata
hivyo alisema kuwa rika linaloongoza kwa ugonjwa huo nikuanzia miaka
mitano kuendelea hadi watu wazima ambapo hadi sasa hawajagundua chanzo
hasa cha ongezeko hilo la ugonjwa wa u.t.i .
Aliongeza
kuwa ingawa kuna viashiria vya sababu vya ugonjwa huo kuwa ni kutoweka
mazingira safi ya vyoo ,mazingira opia ya kujiassaidiua haja ndogo
mahali amabpo si salama kwa afya ya mtumiaji eneo hilo hali ambayo
inapelekea kupata kwa ugonjwa huo.
Sr,Jane
aliongeza kuwa bado pia kuna changamotio ya kujitokeza kwa wananchi
kupima afya zao ili kuweza kujua kama afya ninzuri ama imepeta
maambukizi yoyote ya magonjwa mbalimbali ili kuweza kucukua tahadhari na
kuweza kupata matibabu ya ugonjwa husika.
Mbali
na jitihada za jiji hilo kuweza kupambana na adui maradhi wameunda
mkakati wa kutumia kikosi kazi cha kuweza kukagua mazingira ya wananchi
wake kuangalia namna ya kuweka mazingira safi ili kuweza kuepuka kupata
maradhi na kuweka sheria ndogondogo endapo mtu atakiuka basi apelekwe
kwenye vyombo vya sheria ili kuweza kudhibiti wananchi wakaidi wa
taratibu za kuishi na nchi.
Ameitaka
jamii kwa ujumla kuweza kuwa na taratibu ya kupima afya zao kwani hivi
sasa ugonjwa huo umekuwa ni kikwazo cha utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa
upande wake mwakilishi wa wananchi Bi,Emiliani Msuya aliiomba Serikali
kuweza kutenga fungu la kuweza kuwapa elimu wananchi wake ili kuweza
kuwafundisha namana ya urtunzaji mazingira ili kuweza kuepuka kupata
ugonjwa wa maambukizi ya njia ya mkojo ili kuweza kunausuru kurudisha
nyuma jitihada za kujiletea maendeleo kupitia famili na wananchi wake.
Aliongeza
kuwa wananchi wanatakiwa kuiunda vikundi vidogovidogo ili kuweza
kusimsmiana katika kutunza mazingira na si kusubiri pindi Serikal;i
mpaka ianze kampeni ya upimaji na kuweza kuhamasisha wananchi kupima
afya zao.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia