WATANZANIA WANG'ARA MBIO ZA NGORONGORO MARATHONI 2015


Waziri mkuu Mstaafu ,Fredrick Sumaye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo waandaji buda mfupi kabla ya kuanza kwa mbio za Km 21 Katika gate la kuingilia hifadhi ya taifa ya Ngorongoro,
Waziri mkuu Msaatfu Fredirick Sumaye akikimbia sambamba na rais wa shirikisho la riadha Tanzania,RT,Athony Mtaka(Kushoto kwake) mkuu wa mkoa wa Arusha ,Daud Ntibenda,pamoja na mkuu wa wilaya ya Karatau Omary Kwaang kuashiria kuanza kwa mbio za Ngorongoro Marathoni.
Mbio zikianza rasmi.
Hatimaye wakapatikana wakimbiaji watatu wakaongoza hadi mwisho wa mbio na hawa ni ,Joseph Theofily(katikati),George Gerald (kulia) na Emanuel Giniki.
Mshindi wa kwanza katika Mbio za Ngorongoro Maratahoni 2015 ,Joseph Theofily akimaliza mbio hizo katika uwanja wa Mazingira Bora akitumia muda wa 1:03:09.
Mshindi wa kwanza kwa kina dada Failuna Abdi akihitimisha mbio katika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa 1 :10:25
Mgeni rasmi katika mbio hizo ,Waziri mkuu Mstaafu ,Fredirck Sumaye akiingia uwanjani huku akihitimisha mbio za km 21 .


Mkurugenzi wa Zara Tanzania and Adventures,Zainab Ansel akizungumza na wanahabari katika tamasha hilo.
Meza kuu wakifuatilia mambo mablimbali yanavyoenda uwanjani hapo.
Mkurugenzi wa Zara Tanzania and Adventures,Zainab Ansel akizungumza wakati wa kuhitimisha tamasha la nane la mbio za kimataifa za Ngorongoro Marathoni zilizofanyika Karatu mkoani Arusha.
Baaadhi ya wananchi waliojitokeza katika tamasha hilo.
Rais wa shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza katika tamasha hilo.
Waziri mkuu Mstaafu ,Frerick Sumaye akitoa hotuba yake wakati wa tamasha la nane la mbio za kimataifa za Ngorongoro Marathoni zilizofanyika mwishoni mwa wiki Karatu mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Zara Tanzania and  Adventures,Zainab Ansel akitoa zawadi kwa washindi wa mbio za Km 5 upande wa wasichana.
Waziri mkuu mstaafu ,Fredrick Sumaye akizungumza na mshindi wa kwanza mbio za Km 5 kwa upande wa wasichana aliyemaliza mbio bila ya kuwa na kiatu,Sumaye alimpatia zawadi ya fedha kwa ajili ya kununua kiatu.
Umati wa wananchi ukifuatilia matukio mbalimbali katika mbio hizo.
Mkurugenzi wa Zara Tanzania and Adventures ambao ndio waandaaji wakuu wa mbio hizo,Zainab Ansel akikabidhi zawadi kwa mwakilishi wa Bonite Bottlers ambao pia walikuwa wadhamini wa mbio hizo.
Mkurugenzi wa Zara Tanzania and Adventures ambao ndio waandaaji wakuu wa mbio hizo,Zainab Ansel akikabidhi zawadi kwa mwakilishi wa Exim Bank  ambao pia walikuwa wadhamini wa mbio hizo.
Mkurugenzi wa Zara Tanzania and Adventures ambao ndio waandaaji wakuu wa mbio hizo,Zainab Ansel akikabidhi zawadi kwa mwakilishi wa Marenga Investment ambao pia walikuwa wadhamini wa mbio hizo.
Waziri mkuu mstaafu ,Fredrick Sumaye akikabidhi zawadi kwa mkurugenzi wa Zara Tanzania and Adventures kama mwandaji mkuu wa mbio hizo.
Washindi wa mbio hizo kwa upande wa wanawake,
Waziri mkuu mstaafu ,Fredrick Sumaye akimvisha medali mshindi wa kwanza katika mbio hizo,Failuna Abdi.
Waziri mkuu Mstaafu akiwa katika picha ya pamoja na washindi.
Waziri mkuu mstaafu akimvisha medali ,mshindi wa kwanza katika mbio za km 21 kwa upande wa wanaume ,Joseph Theofily,

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post