BREAKING NEWS

Tuesday, April 28, 2015

MBUNGE NATSE AWATAKA WANANCHI WA KARATU KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

SAM_2291 Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akihutubia wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mazingira bora karatu mjini jana,amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambayo itawapa fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika ockoba mwaka huu (Habari picha na Jamiiblog) SAM_2293 Wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanamsikiliza Mbunge wao akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa mazingira bora karatu mjini SAM_2292 Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse akiwa anasisitiza jambo jukwaani ambapo alisema njia bora ya kuwapiga chini chama cha mapinduzi CCM ni kwa kuhakikisha wananchi wanajiandikisha katika daftari la kudumu huku akidai safari hii ni jino kwa jino hadi ikulu. SAM_2279 Mwenyekiti wa vijana Wilaya ya Karatu John Male alisema lengo lao ni kuwaelimisha wananchi hata wasio wanachama kuhusu umuhimu wakujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura SAM_2282 Diwani wa kata ya Karatu mjini Jublate Mnyenye aonya Redio mbao zinazosambaza habari kuwa anampango wa kuihama chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)adai yeye na chama hicho ni damu damu. SAM_2265 Wananchi wakimshangilia Mbunge wao SAM_2296 Mzee Peter akijichukulia matukio mbalimbali na simu yake ya mkononi SAM_2294 Wananchi wa Karatu wakiwa makini kusikiliza SAM_2304 Mwananchi akieleza kero yake kwa Mbunge wake SAM_2312 Jackine ambaye aliwakilisha wanawake akiuliza swali kwa Mbunge wake juu ya Hospitali za serikali kukosa dawa SAM_2311 Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akiwa anateta jambo meza kuu

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates