Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey,
Badru Ntege (kulia) akimwonyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly
effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya
kwanza nchini Tanzania mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), Nehemia Mchechu mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi huo
uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena.(Picha zote
na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),
Nehemia Mchechu (kushoto) akipitia kurasa mbalimbali za kitabu hicho kabla
ya uzinduzi rasmi. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin
Covey, Badru Ntege.
Mwezeshaji wa Franklin Covey, Alice Levora akichambua
kwa ufupi tabia 7 zilizomo kwenye kitabu hicho kwa wageni waalikuwa (hawapo
pichani) kabla ya uzinduzi rasmi.
Na
Mwandishi wetu
UWEKEZAJI mkubwa unatakiwa kufanywa katika eneo la
raslimali watu, kama taifa hili linahitaji kuondokana na malalamiko kuhusu
maendeleo na ajira.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
Nehemia Mchechu wakati akizindua tafsiri ya kiswahili ya kitabu cha "The 7
Habits of Highly effective people" kilichoandikwa na Mmarekani, Stephen
Covey.
Hii
inakuwa tafsiri ya kwanza ya kitabu hiki kwa lugha za asili zinazotumika
bara la Afrika .
Alisema malalamiko mengi kuhusiana na taifa kuwa na
raslimali nyingi na umaskini kuendelea kuwepo yanatokana na kutoendelezwa
kwa raslimali watu kwa lengo la watu kujitambua, kutambua wanachotaka na
kusababisha kiwepo.
Alisema inasikitisha kuona kwamba watanzania wengi
wanalalamika kuhusu hali ngumu kumbe ilhali wao huenda ndio wakawa sababu
za matatizo hayo ya ukosefu wa maendeleo.
Alisema ni vyema watanzania wakajenga utamaduni wa
kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika kwa
kuwa vitabu hivyo vina tafiti nyingi za miaka mingi ambazo watanzania
wakitumia kwa muda mfupi watafanya mabadiliko katika maisha
yao.
Alisema uwapo kwa tafsiri ya Kiswahili kwa moja ya
vitabu vyenye sifa kubwa duniani katika masuala ya menejimenti na ambacho
kimekuwa katika 20 bora za vitabu duniani kwa miaka 20, kutasaidia
watanzania wengi kujiangalia na kujifunza kuwa na dira na nidhamu ya
kutekeleza yale ambayo wanayafikiria.
Alisema kwamba ari ya kusoma kazi mbalimbali kutasaidia
watanzania kuwa na upeo mpana wa kujituma na kuwa na nidhamu ya malengo
wanayostahili ya kufikia kwa muda mfupi na kwa ufanisi
mkubwa.
Tafsiri hiyo ya kitabu ambayo imewezeshwa na Baraza la
Kiswahili nchini Tanzania (BAKITA) na imeandaliwa taasisi ya ushauri wa
masuala ya maendeleo ya raslimali watu (NFT).
NFT
ambayo makao makuu yake yapo mjini Kampala, Uganda ina matawi Kenya,
Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
Wajibu
wake mkubwa taasisi hiyo ni kukabilina na changamoto mbalimbali za
wafanyakazi kwa kutoa mafunzo yenye kutengeneza manufaa kwao na kwa
menejimenti ya uhuru na kutegemeana katika kufanikisha maono ya taasisi
husika.
Kutumika kwa kitabu hicho chenye kurasa 380 kwa kuangalia
tabia zenye manufaa kunatokana na haja ya kubadilisha mfumo wa uongozi na
ushirikishaji wenye lengo la kuchochea kutegemeana katika kuleta
ufanisi.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), Nehemia Mchechu (kulia) na Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili
Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa
lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa (wa pili kushoto) pamoja na wadau
wengine wakifuatilia uchambuzi wa kitabu hicho.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey,
Badru Ntege akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
kuzungumza na wageni waalikwa.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), Nehemia Mchechu akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha
"The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya
Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ambapo alitoa rai kwa
Watanzania kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa
mwanga wa kujituma na kuwajibika.
Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania
(BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha
ya Kiswahili, Vida Mutasa akielezea changamoto alizokutana nazo wakati wa
kutafsiri kitabu hicho.
Pichani ni kikundi cha burudani kutoka Tanzania House
of Talent (THT) wakitumia sanaa "Choreograph" kuzindua rasmi kitabu cha
"The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya
Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
Sasa kimezinduliwa rasmi.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), Nehemia Mchechu akipokea kitabu cha "The 7 Habits of highly
effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya
kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na
maeneo ya kazi kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin
Covey, Badru Ntege (kulia). Katikati anayeshuhudia tukio hilo ni Mtafsiri
mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa
tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), Nehemia Mchechu akionyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly
effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya
kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na
maeneo ya kazi kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo
pichani).
Kutoka kushoto ni Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la
Kiswahili Tanzania (BAKITA), Vida Mutasa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT
Consult/Franklin Covey, Badru Ntege, Mkurugenzi wa NFT Consult, Nambie
Kiwanuka pamoja na Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey
Tanzania, Joan Ajilong.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), Nehemia Mchechu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NFT
Consult/Franklin Covey Tanzania.
Mratibu wa shughuli ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7
Habits of highly effective People"kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili
kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kutoka JB's PR & Events, Babbie
Kabae akifafanua jambo kwa wageni waalikwa (hawapo
pichani).
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa
ambao ni maafisa rasilimali watu na wadau kutoka makampuni mbalimbali
waliohudhuria uzinduzi huo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia