Mbio za nusu
Marathon kilomita 21 za Ngorongoro zenye
lengo la kutokomeza ugonjwa wa Malaria zinatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 18
ya mwezi huu wilayani Karatu na kuwashirikisha wakimbiaji nguli kutoka ndani ya
nchi na nchi jirani.
Mbio hizo
zinazofanyika kwa msimu wa nane ambapo mshindi wa mbio hizo mwaka jana Alphonce
Modest nae pia anatarajiwa kutetea ubingwa wake kwenye mbio hizo za mwaka huu.
Kwa mujibu
wa mratibu wa mbio hizo Mwta Petro alisema kuwa zawadi zimeboreshwa katika mbio
hizo kwa wahsindi wote kwani mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha
shilingi million 1 na laki mbili huku mshindi wa pili akijinyakulia sh.laki
sita na watatu sh.laki nne.
Petro
alisema kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa na mbio za kilometa tano kwa makundi ya
wafanyakazi kutoka taasisi mbali mbali na washindi watapata fursa ya kutembelea
mbuga ya wanyama ya Ngorongoro huku pia kutakuwa na mbio za kilometa 2.5 kwa
vijana na wanafunzi ambao wanaandaliwa kuwa wakimbiaji hapa mbeleni.
“Tunatarajiwa
mbio hizo kuwa kubwa hapo baadae kwani zimeonyesha kuwa na mvuto kwa washiriki
mbali mbali kutopka ndani na nje ya nchi kwani kwa mwakan huu kumekuwa na
wakimbiaji kutoka mataifa ya marekani,Norway na Sweden na nchi za ukanda wa
Afrika ya Mashariki na Malawi pia wamethibtisha kushiriki mbio hizi”alisema
Meta.
Akawataka
wanariadha mbalimbali kuanza kujiandikisha kwani vituo teyari vimeshafunguliwa
kwenye mikoa ya Arusha,Manyara,Kilimanjaro na wilayani Karatu huku akiwataja
wadhamini wa mbio hizo zilizokuwa zikidhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi
ya Tigo kuwa ni Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola na Zara Charity.