Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio
jamii ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha
wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha
mafunzo ya masoko na mpango biashara kwa viongozi wa redio jamii nchini
wakati kuhitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi wa Shirika la
Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya
Tehama na Mawasiliano iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu
Sayansi na Utamaduni UNESCO ambayo imefanyika katika kituo cha Redio jamii
Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
Na
Mwandishi wetu, Mwanza
WAMILIKI wa redio za jamii wametakiwa kujenga taswira
njema za redio zao ikiwa wanataka redio zao zitamanike na kutumiwa na
wadua mbalimbali wa maendeleo nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati
(ASMET), Ramadhan Ahungu.
Akizungumzia malengo ya warsha hiyo na madhumuni yake
alisema kwamba kuwapo kwa mpango wa biashara ndani ya redio hizo hakutakuwa
na maana kama wasipozingatia ujenzi wa taswira utakaowafanya wadau kuvutiwa
na redio hizo.
Alisema kuna umuhimu wa suala hilo kwani kusipojengeka
kwa mahusiano bora kati yake na jamii, watu binafsi na taasisi za kiraia
zenye malengo tofauti katika kuhudumia wananchi, redio hizo hazitakuwa na
biashara ya kufanya.
Ahungu
pamoja na kusifia mtindo uliotumika kuwezesha redio hizo kuandaa mipango
kazi ya biashara yenye lengo la kusimamia masoko na fedha alisema warsha
imefanikiwa kuwaweka karibu zaidi na wadau wamiliki wa vyombo
hivyo.
Warsha
hiyo ni hitimisho ya awamu ya kwanza kwa ufadhili wa mradi wa Shirika la
Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo redio za jamii katika matumizi
ya Tehama na mawasiliano inayoratibiwa na Shirika la Kimataifa la Elimu
Sayansi na Utamaduni UNESCO iliyofanyika katika kituo redio cha Sengerema
Telecentre mkoani Mwanza.
Alisema katika warsha hiyo wamiliki hao walijifunza
uandaaji wa mipango ya biashara, kutunza fedha, utafutaji masoko, uhakiki
wa mipango ya biashara na vipindi vya redio kwa lengo la kuona namna ya
kuvifanya kuleta biashara.
Naye
Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Marco Mipawa
akizungumzia mafunzo hayo alisema yamemsaidia sana katika kuhakikisha
kwamba kituo chake kinakuwa bora na kinachovutia
watangazaji.
Alisema mafunzo hayo yamewafanya wajitambue kwani
yamefanyika mfululizo kwa mara 5 na kuwafanya
wabadilike.
Aidha
Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina
Lweramula alisema kwamba anashukuru mafunzo kwa kuwa yamewafanya kuondoa
mawazo vichwani na kuweka mipango kazi katika karatasi na kuwezesha
wafanyakazi nao kufuatilia.
Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani
Karagwe, Adelina Lweramula akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo
yaliyomalizika jana kwenye kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre
mkoani Mwanza.
Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya
Shinyanga, Marco Mipawa akiuliza swali kwa mkufunzi wa warsha ya mafunzo ya
masoko na mpango biashara (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha warsha ya
awamu ya kwanza inayofadhiliwa na mradi wa SIDA kwa kushirikiana na UNESCO
iliyomalizika jana katika kituo cha Redio Jamii cha Sengerema-Telecentre
mkoani Mwanza.
Pichani juu na chini ni Viongozi wa Redio Jamii
nchini walioshiriki mafunzo ya masoko na mpango biashara yanayofadhiliwa na
mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo
katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano na kuratibiwa na Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ikiwa ni hitimisho la
warsha ya awamu ya kwanza ya mradi huo yaliyofanyika katika kituo cha Redio
Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio
jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na
wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu akiendelea kuwapiga msasa viongozi hao
namna ya kutafuta masoko na kuboresha mpango
biashara.
Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio
jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na
wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu (kulia) akibadilishana mawazo na Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi,
Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (wa pili kulia) wakati
wakijiandaa kwa zoezi la picha ya pamoja. Kushoto ni Mshauri na Mkufunzi
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa vituo vya
Redio Jamii nchini.
Picha ya pamoja ya Wakufunzi na washiriki wa warsha
ya mafunzo ya masoko na mpango biashara iliyomalizika jana katika kituo cha
Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia