WAPAGAZI WATAKIWA KUJIUNGA NA NHIF

 Makamu Mwenyekiti wa chama cha wapagazi nchini(TPO) Loshiye Mollel
akizungumza katika mkutano wa wapagazi na mfuko wa NHIF mkoa wa Arusha

 Baadhi ya wapagazi wakiwa mkutano wao wa kanda mjini Arusha.ukumbi wa
golden View.

 Mfamasia wa NHIF Mshindo Msulle akitoa mada huu ya huduma za NHIF hasa
maduka ya dawa ambayo wanaweza kupata madawa pindi watakapokosa hospitali.
Afisa matekelezo wa mfuko wa bima ya afya mkoa wa Arusha, Desderius
Buhiye alitoa elimu juu ya huduma zinazotolewa na NHIF


Zaidi ya vijana  20,000 wanaofanyakazi ya kubeba mizigo ya
watalii,(wapagazi) katika Mlima Kilimanjaro na Meru ,wametakiwa kujiunga na
mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ili kujihakikisha huduma bora ya afya .
Meneja wa NHIF mkoa Anisia Ngweshem alitoa wito huo , katika mkutano wa
Wapagazi , ulioandaliwa na chama cha wapagazi(TPO),uliofanyika katika
ukumbi ya Golden View jijini hapa.
Ngweshem alisema, NHIF ina huduma bora za kuwapatia matibabu watanzania
ikiwepo huduma mpya ya kulipia kwa mwaka 76,800 makundi maalum.
Akizungumzia huduma za afya kwa wapagazi, Mwenyekiti wa bodi ya TPO Alex
Lemenge alisema chama hicho, kinaandaa utaratibu wa kuhakikisha wapagazi
wote wanajiunga na mifuko ya bima za afya.
Alisema utaratibu huo, utaondoa matatizo ya wapagazi kufariki kwa kukosa
huduma bora za afya kutokana na kazi ngumu wanayofanya kubeba mizigo ya
watalii na kupanda milima.
Awali Makamu mwenyekiti wa TPO, Loshiye Mollel aliomba serikali kuwaunga
mkono wapagazi ili waweze kupata maslahi bora ambayo ndio yatawapatia
huduma bora za za afya.
"tumekuwa na mgogoro na makampuni ya utalii kwa zaidi ya mwaka sasa,
tunaomba yatekeleze maelekezo ya serikali kulipa ujira kwa siku kati ya Tsh
12,000 hadi 15,000 lakini hadi sasa ni makampuni 28 tu kati ya Zaidi ya 400
ndio yanalipa"alisema.
Katika mkutano huo, wapagazi waliunga mkono, mpango wa kujiunga na NHIF
huku wakitaka uongozi wa TPO kwa kushirikiana na taasisi nyingine
kushinikiza malipo bora kwa kazi yao.
kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post