Ticker

6/recent/ticker-posts

WARWANDA WAPONGEZA SEREKALI YATANZANIA KWA KUANDAA MAONYESHO YA MADINI NA VITO

WADAU wa Madini ya Vito kutoka nchini Rwanda wameipongeza  serikali ya
Tanzania kwa maandalizi mazuri ya maonyesho ya madini ya vito
yaliyofanyika jijini Arusha,hususani  suala la usalama na kuahidi
kuwashawishi wenzao wa Rwanda waje kushiriki maonyesho hayo.

Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa kampuni ya madini ya nchini
Rwanda,Rugamba Mining , Robert Rugamba , wakati wakizungumza na gazeti
hili jijini hapa,kuhusiana na  mwenendo wa maonyesho hayo
yaliyofanyika kwa mara ya nne jijini hapa,ambapo kampuni yake imekuwa
ikishiriki kila mwaka.

Alisema tofauti na mwaka jana mwaka huu,maonyesho yameboreshwa zaidi
kwa kuimarisha ulinzi na kufanya biashara zinazofanyika kuwa za
uhakika zaidi.

‘’Kwa kweli sio siri mwaka huu serikali imejitahidi sana sisi
waonyeshaji tumefurahishwa na usalama uliopo ,mwaka jana tulifanyia
nje kwenye hela ,lakini mwaka huu tunatumia vyumba maalaumu’’alisema.

Alitoa wito kwa serikali kupitia waandaaji wa maonyesho hayo ambao ni
chama cha wafanyabiashara wa madini,TAMIDA kuyaongeza muda ili
washiriki waje kwa wingi tofauti na sasa muda wa siku tatu walidai ni
mfupi sana.

Aliahidi kuwashawishi wafanyabiashara wenzake wa madini waliopo nchini
Rwanda waje Arusha ,Tanzania kuleta madini kwa kuwa usalama ni wa
uhakika na kwamba wageni mbalimbali ni wengi ,hivyo uhakika wa kuuza
ni mkubwa.

Alisema madini waliokuwa wakiuza katika maonyesho hayo  ambayo ni
maarufu sana nchi kwao ni pamoja na Wolfram,Coltan na Cassitente

Post a Comment

0 Comments