Mwenyekiti wa Kariakoo Family Foundation (KFF) Mohamed Bhinda
akiongoza kikao cha Kamati ya Utendaji katika kuandaa rasimu ya katiba ya
chama hicho kinachotarajiwa kusajiliwa hivi karibuni kama taasisi
isiyo ya kiserikali kwa nia ya kukutanisha upya wadau wote waliozaliwa,
walioishi na wenye asili ya Kariakoo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es
salaam. Mkutano huu umefanyika leo jioni Kinondoni Studio. Kulia kwa Bhinda
ni katibu wa chama hicho Senpai Wahid
Mtunza hazina wa KFF Yahaya Sameja akielezea namna chama
hicho cha jamii ya wana Kariakoo kitavyoweza kujiendesha kwa njia za ada,
michango na misaada ya wafadhili katika kuendeleza wanachama, ikiwa ni
pamoja na kusaidiana katika shida na raha. Kushoto ni Mwenyekiti wa KFF
Mohamed Bhinda na kati ni Makamu Mwenyekiti Tatu
Lumelezi
Wana KFF wakipata mlo wa mchana wakati wa
mapumziko
Jopo la
kamati ya utendaji ya KFF baada ya mkutano