Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha Programu ya Uongozi na
Maadili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es
salaam leo. Kushoto kwake ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na
kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa shughuli tayari
kuzindua Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya
Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Mkuu wa Chuo
hicho Profesa Shadrack Mwakalila.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsimika rasmi Mzee Pius Msekwa kuwa
Mwenyekiti wa Kibweta cha Mwalimu Nyerere cha Uongozi na Maadili wakati
wa uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi katika Chuo cha
Kumbukumbu ya Nyerere Kigamoni jijini Dar es salaam leo.