Vilabu nane kutoka jijini Arusha zinatarajia kupimana
uwezo katika mchezo wa Taekwondo katika ligi maalum inayotarajiwa kutimua vumbi appril 25 mwaka
huu katika viwanja vya Complex vilivyoko njiro jijini hapa kwa ajili ya
kuchagua wachezaji watakaowakilisha mkoa katika mashindano ya kitaifa ya Mei
mosi.
Vilabu vya
Taekwondo vinavyojifua katika viwanja mbali mbali kwa ajili ya mashindano hayo
ni pamoja na Tripple ‘A’, Naura, kili, Kijenge pamoja na Meru, Chishwea, M.S na
AICC ambapo kila mchezaji anasaka nafasi ya kuchaguliwa kuunda timu ya mkoa
itakayo wakilisha katika mashindano hayo ya mei mosi yatakayofanyika jijini
hapa may 1 mwaka huu.
Akizungumza
na gazeti hili, katibu mkuu wa shirikisho la mchezo wa Taekwondo Tanzania,
Shija Shija alisema kuwa wametoa nafasi kwa vilabu mbali mbali kujiandaa na
mashindano ya mei mosi itakayosaidia kuendelea kuwanoa wachezaji katika
mashindano ya kitaifa baadae watakapokua wanachagua timu itakayowakilisha nchi
kwenye mashindano ya Afrika hapo septemba kule Brazavile, Congo.
“Mashindano
haya ni ya wazi kwa vilabu vyote Tanzania kushiriki ili kuwanoa zaidi wachezaji
wao na tutaandaa mashindano mbali mbali kwa wachezaji kutoka ndani na nje ya
nchi lengo ni kuwajenga wachezaji wetu kimashindano zaidi wazidi kuleta medali
mbali mbali za kimataifa kama mashindano yaliyopita”
Mkurugenzi
wa ufundi wa mchezo wa Taekwondo mkoa wa Arusha Richard Kitolo aliliambia
gazeti hili kuwa wameandaa mashindano yao maalum ya ndani ili kuchagua
wachezaji wazuri watakaoshiriki michuano ya mei mosi ambayo wao watatayatumia
mashindano hayo kuchagua timu ya mkoa
itakayowakilisha katika mashindano ya kitaifa baadae.
“Sisi
wenyewe tumeamua kuandaa mashindano yetu ya ndani kabla hayo ya mei mosi
hayajafika ili kuanza mchujo wa wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kupambana na
mchujo wa pili tutaufanya kwenye mashindano hayo ya mei mosi kupata timu ya
mkoa”
“Sisi
mashindano haya kwetu ni mazuri na tutatumia kuchagua timu ya Mkoa, lakini changamoto kubwa inayotukabili kwa sasa
ni wachezaji wachache kutokana na wazazi kutoruhusu watoto wao kushiriki katika
mchezo hasa wasichana hivyo tuwaombe wazazi wawaruhusu watoto kushiriki katika
michezo kama hiyo kuwajenga kiakili na afya pia”
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia