Mratibu wa Kambi ya matibabu Arusha katika kituo cha kutoa huduma kwawanawake
(MMC)kilichopo mkabala na Hoteli ya Impala, ambapo ushauri huo
unatolewa, Austin Makani akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio
wa madaktari bingwa kutoka India kwaajili ya kuwaona wagonjwa wenye
matatizo ya Moyo,Tumbo,Upasuaji wa saratani,Mishipa ya fahamu na uti wa
mgongo,Shida za Figo,Mifupa,upasuaji wa jumla na upasuaji wa kupunguza
uzito,zoezi hilo litafanyika kwanzia tarehe20-22
Madaktari bingwa kutoka India
Daktari
bingwa kutoka India katika hospitali ya Apollo Abhijit Singh
akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha
katika kituo cha MMC Health
Wagonjwa wakiwa wanapatiwa vipimo mbalimbali
Atul Behll ambaye pia ni daktari bingwa kutoka India akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari
Mgonjwa aliyekuja kupata huduma akiwa anasaidiwa na wahudumu wa kituo hicho
Wagonjwa wakiwa wanasubiria kupata huduma
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kazini
MADAKTARI
bingwa kutoka hospitali ya SPS Apollo iliyopo Ludhiana nchini India
wamewasili nchini na kuanza kutoa huduma ya ushauri bure kwa magonjwa makubwa ambayo yamekuwa yakiwasumbua watu wengi na kuwalazimu kwenda kutibiwa nchini India.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kutoa huduma kwa wanawake (MMC) ambapo ushauri huo unatolewa, Mratibu wa Kambi hiyo ya matibabu Arusha, Austin Makani alisema kuwa , madaktari bingwa hao wanatoa ushauri kwa wagonjwa wenye matatizo ya Figo , Moyo, tumbo, saratani, mishipa ya fahamu, uti wa mgongo, upasuaji wa kawaida na wa
kupunguza uzito.
Austin alisema kuwa, ujio wa madaktari hao watano kutoka nchini India umeratibiwa na kituo cha kutoa huduma kwa wanawake (MMC) kwa kushirikiana na hospitali ya SPS Apollo iliyopo Ludhiana nchini India na wamefikia hatua hiyo baada ya kugundua kuwa wagonjwa wengi wanaoenda kutibiwa nchini India wanasumbuliwa na magonjwa hayo.
Alisema kuwa, uwepo wa madaktari hao bingwa kwa siku tatu utasaidia sana wananchi wa jiji la Arusha kufika na kupewa ushauri bure juu ya magonjwa yanayowasumbua na hivyo kuokoa gharama ya kusafiri hadi nchini India kufuata huduma hizo.
‘hapa sisi wanachofanya madaktari hawa bingwa ni kusikiliza wagonjwa na baada ya kupata maelezo wanapata ushauri bure wa kwenda kupima kulingana na ugonjwa alionao na baada ya kurudisha majibu ndipo tunamwandikia dawa ya kutumia na kama ugonjwa wake unahitaji kutibiwa India tunampunguzia gharama kidogo ya kwenda kutibiwa India ‘alisema
Austin.
Alisema kuwa, uwepo wa kambi hiyo ya matibabu jijini Arusha unatoa fursa pia kwa wagonjwa waliokuwa wakatibiwe nchini India kutokana na magonjwa yanayowasumbua na kuweza kupata ushauri wa haraka na wakti mwingine kuepuka gharama za kusafiri.
Wakizungumza katika kituo hicho, Madaktari hao bingwa ,Abhijit Singh na Atul Behll kutoka hospitali ya SPS Apollo India walisema kuwa ,changamoto kubwa iliyopo katika nchi za kiafrika ni watu wengi kutokuwa na utamaduni wa kwenda kupima afya zao ,hivyo aliwataka
wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kufika kwa wiki ili kupata ushauri juu ya afya zao.
Walisema kuwa,nchini India kuna watanzania wengi wanaopata matibabu kutokana na magonjwa yaliyotajwa ,hivyo wakaona kuna umuhimu mkubwa kwa wao kuwafikia na kuweza kutoa ushauri bure na hatimaye kupunguza gharama za kwenda nchini India.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia