BALOZI ADADI :AWATAKA WANAFUNZI WILAYANI MUHEZA KUJIKITA KWENYE MASOMO YA SAYANSI


Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi
Rajabu akionyesha moja kati ya vifaa vya maabara ambayo wilaya ya Muheza imepatiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari wilayani humo juzi wakati alipokwenda kukabidhi kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Luiza Mlelwa kushoto ni Afisa Elimu Sekondari wilaya hiyo  Julitha Akko
Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari
Muheza High School,Luqman Mustapha akimueleza Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu juzi namna wanayotumia vifaa vya maabara walivyopatiwa wakati alipokabidhi vifaa vya maabara  kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa nchini

MBUNGE wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi wa shule za Sekondari wilayani humo kuongeza bidii ikiwemo kujikita kwenye masomo ya sayansi ili kuweza kuendana na sera ya viwanda ilivyopo hapa nchini.
Balozi Adadi aliyasema hayo jana wakati alipokabidhi vifaa vya maabara  kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya ElimuSayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa chini.

Alisema vifaa hivyo ambayo vimetolewa katika shule 7 kati ya 24
wilayani humo vitakuwa ni chachu ya wanafunzi kuweza kufikia malengo yao ya kufanya vizuri katika masomo yao katika hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya Muheza.

“Jambo hilo ni nzuri na hasa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kutaka vifaa hivyo vikabidhiwe katika shule ambazo zitakuwa zimekamilisha ujenzi wa maabara na vitaweza kuwapa mwanga mzuri kusoma kwa bidii “Alisema.

Alisema ni jambo la ajabu iwapo vifaa ambazo vimekabidhiwa vitatumika vibaya kitendo ambacho kitakwamisha juhudi za serikali za kutaka wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo ili waweze kuendana na sera ya viwanda.

“ Vifaa hivi ambavyo mmekabidhiwa leo hii vinagharama kubwa hivyo niwaombe ndugu zangu mhakikishe mnavitunza ili viweze kutumika katika matumizi yaliyokusudiwa lakini pia niwatake wanafunzi mhakikishe mnasoma kwa bidii “Alisema

Mbunge huyo alisema lipo tatizo la kubwa la kutokuwepo vifaa vya maabara katika shule nyingi za sekondari hapa nchini jambo ambalo limeanza kupatiwa ufumbuzi na serikali ya awamu ya tano kupitia wizara ya elimu ili kuona namna ya kulimaliza.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Afisa elimu sekondari wilaya Muheza Julitha Akko amewaagiza walimu wakuu wa shule za sekondari zilizopatiwa vifaa hivyo kuacha tabia ya kufungia ndani ya makabati na badala yake vitumike kama ilivyokusudiwa.

Aidha alisema kuwa lazima kuwekwe utaratibu wa namna ya kuvitunza vifaa hivyo na kuagiza visitumike kinyume na makusudio yake na kuwataka wanafunzi waelekeze nguvu zao kwenye masomo ili kuongeza wataalamu wengi.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Muheza(Muheza high school) Alex Birumo alisema yapo mategemeo makubwa ya kuongeza ufaulu hasa kwa masomo ya sayansi kutokana na kupatikana kwa vifaa hivyo ambavyo wanafunzi walikosa fursa kwa miaka mingi kujifunza kwa vitendo.

“Shule yetu hii ni ya masomo ya sayansi ya michepuo ya PCB NA CBG na ni ya kidato cha tano na sita unapokuwa na wanafunzi zaidi ya 150 unawafundisha bila ya vifaa vya maabara kiukweli mafunzo yetu kwa wanafunzi hao yahakuwa na tija”Alisema
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post