Ticker

6/recent/ticker-posts

TANZANIA YAKANA KUINGILIA UCHAGUZI WA KENYA.




Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanian imekanusha madai kwamba inaisaidia chama cha upinzani nchini Kenya cha Muungano wa NASA ili kuwekwa kwa kituo cha kuhesabia kura nchini Tanzania.

Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Hassan Abbas amesema kuwa si sahihi kuiunganisha Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka huu nchini Kenya.

“Suala hili la kujaribu kuiunganisha nchi inayopenda amani ya Tanzania kuhusika kwenye Uchaguzi Mkuu wa majirani zetu ni kosa kubwa lisilofikirika.”

Shutuma hizi zimeibuka baada ya kuzagaa kwa taarifa kwamba mgombea wa upinzani Raila Odinga kupitia Muungano wa NASA kuwa wamefanya mpango wa kuweka kituo cha kuhesabu kura maeneo ya Kigamboni jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Alliance, Ekuru Aukot amesema kuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kinyume na Katiba ya Kenya na Uhuru wa nchi hiyo.

Msemaji wa Serikali ya Tanzania aliendelea kusema kwamba: “Nina wasiwasi na taarifa kwamba Muungano wa NASA una mpango wa kuweka kituo cha kuhesabu kura hapa Tanzania. Suala hili ni sawa na kuidharau Katiba yetu na kudhalilisha Uhuru wa nchi yetu,” amesema Abbas.

Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba hatua hiyo kutoka Muungano wa upinzani umesababisha mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili. Imesemekana kwamba kwa sababu ya jambo hili, wakubwa serikalini wamekuwa wakiitaka Serikali ya Tanzania kutoa kauli hadharani kuzungumzia suala hili.

‘HAKUNA MPANGO WOWOTE ULIOWEKWA KATI YA MAGUFULI NA RAILA’
Katika mahojiano na kituo cha redio cha Jambo, Raila amesema kwamba chama tawala cha Jubilee kina wasiwasi wa kushindwa kwenye Uchaguzi Mkuu kwahiyo wakaamua kuzusha “propaganda” hiyo kuhusu kituo cha kuhesabu kura nje ya Kenya.

“Sielewi kwa nini watu wanafatilia sana urafiki wangu na Rais wa Tanzania, John Magufuli,” alisema.

“Familia zetu ni rafiki, na si yeye tu bali hata Rais wa Uganda Yoweri Museveni ni rafiki yangu wa muda mrefu. Urafiki wangu na yeye unazidi urafiki kati ya Museveni na (Rais) Uhuru,” alisema.

Raila ameongeza kuwa yeye ana urafiki na viongozi wengi wa Afrika wakiwemo Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Nana Akufo-Addo wa Ghana.

“Hamna mpango wowote kati ya Magufuli mimi. Sisi ni marafiki tu. Chama cha Jubilee kina njama za kupanga matokeo ya uchaguzi, ndio sababu wanakuja na mawazo yasiyo na maana kabisa.”

Mgombea huyo wa Urais kwa tiketi ya Muungano wa NASA amesema kuwa Muungano huo una mpango wa kuwa na kituo chao ambacho watajumlishia kura zake zote na kuzilinganisha na zile zitakazokuwa zinahesabiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Kenya, IEBC.

“Wana wasiwasi wa nini? Nini cha ajabu sana kuhusu kuhesabu kura zako mpaka Serikali nzima iwe na wasiwasi? Eti NASA itaenda kuhesabia kura zake nchini Tanzania…tatizo liko wapi?” aliuliza.

“Kama IEBC itatangaza matokeo sahihi, kwanini wanaohaha wawe ni watu wa Jubilee? Kwanini wawe na wasiwasi wa sisi tunaenda kuhesabu wapi kura zetu?

“Wao wanataka yuweke vituo hivyo hapa ili waweze kuvivamia na kuharibu mashine zetu za kuhesabia. Wajue kwamba tunazo nyingi. Hata kama watavunja mashine moja au mbili…tutakuwa tumejiandaa,” alisema Raila.

Post a Comment

0 Comments