Mwanasheria Arthur Mbena kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) akiwa katika maonyesho ya 41 ya biashara Kimataifa sabasaba. sabasaba jijini Dar es salaam. |
Bango la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini lenye maelezo namna ya kutambua bima kama ni halali au ni feki kama maelezo yanavyosomeka hapo |
Wa kwanza kushoto ni Mwanasheria Arthur Mbena akiwana Paul Abdiel ambae ni Afisa Mchambuzi (Bima)kutoka (TIRA)Makao makuu Dar es salaam wakiwa katika maonyesho ya 41 ya biashara Kimataifa sabasaba. |
Mamlaka ya
usimamizi wa Bima nchini( TIRA)imetoa rai kwa wananchi kutumia mfumo wa
TIRA MIS ambao utamsaidia mteja kutambua bima za vyombo vya moto zenye
uhalali au feki kwa kutumia mfumo wa kieletroniki.
Hayo yamesemwa na mwanasheria Arthur Mbena ambapo
amesema kuwa mtu yeyote yule ambae atakamatwa na bima feki sheria
itafuata mkondo wake, ameainisha njia ambazo mtu anaweza kutambua bima
yake kama ni feki ama halali kwa kutumia simu ya mkononi( smart
phone)kutumia mtandao http/mis.tira.go.tz,google unadownlod tira mis.
Aidha
amesema kuwa kazi kubwa ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini ni kuwa
msimamizi wa sekta ya Bima mwenye kiwango kinachokubalika
Kimataifa,kuendeleza ,kukuza masoko ya Bima imara,shirikishi lenye
kuthamini usawa na utendaji mahiri,kwa manufaa na kulinda maslahi ya
wateja.
Kwa upande wake Afisa Mchambuzi (Bima)kutoka (TIRA) Paul Abdiel amesema
kuwa mamlaka hiyo inafanya shughuli zake kwa weledi, kuwapa kipaumbele
wateja ,ushirikiano ,kuwajibika ,pamoja na kuaminika na uwazi
Amewataka
wateja wa Bima za vyombo vya moto kuwa makini pale wanapokatiwa Bima
hizo wazihakiki na kuhakikisha kama ni halali ama la.