Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence
Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya
kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania
wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na
Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk.
Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka
Islam (kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence
Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya
kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania
wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na
Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk.
Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka
Islam (kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo,
Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT akijadili jambo katika mjadala wa wadau wa ICT,
wengine ni Robert Madziva- Maxcom Africa (kulia) na Chambi Chachage wakiwa
katika mjadala huo.[/caption] Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo,
Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na
wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Chambi
Chachage-Udadisi Blog, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT pamoja na Robert Madziva-
Maxcom Africa wakiwa katika mjadala huo. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jamii Media, Asha
Abinallah akizungumza na washiriki wa kongamano la wadau wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania.[/caption]
KAMPUNI ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya
Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini
Uganda imefanya kongamano la kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania ikiwa ni kujadili masuala mbalimbali ya
huduma za habari na mawasiliano pamoja na kuangalia namna ya kulinda usiri
wa taarifa za wateja wanaotumia huduma hizo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello alisema kongamano hilo limekuwa na
matokeo chana baada ya wadau kujadili masuala mbalimbali ya ICT lengo
likiwa kuboresha zaidi huduma hiyo na usalama kwa watumiaji. Alisema wadau
wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za
kusimamia huduma nzima ya ICT lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za
maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa huduma
za ICT.
Alisema wadau wengi katika kongamano hilo walihoji kitendo cha Sheria ya
Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) kuanza kutumika bila ya
uwepo wa kanuni jambo ambalo limewapa ugumu hata watekelezaji na wasimamizi
wa sheria husika. Mkurugenzi huyo aliongeza Jamii Media itaendelea kusaidia
kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo
bloggers ili kuona wanakuwa na uelewa na matumizi mazuri ya mitandao yao
kupunguza mkanganyiko kwa wanufaika.
Maria Sarungi (kushoto) Mkurugenzi Uzalishaji
kutoka 'Compass Communications Ltd' akiongoza majadiliano kwenye kongamano
hilo Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo,
Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na
wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kushoto ni Robert Madziva- Maxcom
Africa wakifuatilia mjadala huo
Jamii Media, CIPESA Wakutanisha Wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ICT
bywoinde
-
0