Mhe. Mary Nagu (Mb), Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la Mama shujaa wa Chakula, akifanya ufunguzi wa Kongamano hilo lililofanyika Dodoma.
Bi.Jovitha Mlay, Meneja wa Kampeni kutoka Shirika la Oxfam Tanzania
akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula
linalofanyika mjini Dodoma.
Aliyewahi kuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa
wa ChakulaSister Martha Waziri, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa
wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Pili kishinje Itamba, aliyewahi
kuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula akizungumza wakati
wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Evelyn Kagoma akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Anna Oloshuro, aliyewahi
kuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula akizungumza wakati
wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Shughuli mbalimbali zikiendelea wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Eluka Kibona kutoka Oxfam akiwasilisha mada wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Waliowahi kuwa washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula
wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa
Chakula linalofanyika Dodoma.
Neema Hilonga(wa katikati) aliyewahi kuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa
Chakula akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mhe. Mary Nagu (Mb), ( Kulia)
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Uvuvi (kulia),
Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Oxfam Tanzania, Francis Odokorach
(Kushoto) wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula
linalofanyika Dodoma.
Picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Kongamano la Mama Shujaa wa
Chakula lenye lengo la kuwakutanisha washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula kwa
Msimu wa kwanza hadi wa tano(2011-2015) wamekutana mjini Dodoma kwa lengo la
kuangalia Ajenda mpya ya Mama shujaa wa Chakula kuhusiana na Kilimo na Usalama
wa Chakula.
Akizungumza leo mjini Dodoma
Meneja wa Kampeni, Jovitha Mlay alisema hii ni mara ya kwanza kufanya kongamano
hilo ambalo limewakutanisha washiriki zaidi ya 50 kutoka mikoa mbalimbali
nchini Tanzania.
Alisema kongamano hilo pia
limewakutanisha washiriki hao kama sehemu ya kuangalia na kushawishi serikali
katika masuala ya kisera,kibajeti na kimkakati yanayohusiana na kilimo
hususani kwa wanawake wazalishaji wadogo wa chakula na wataangalia uzoefu
wa washiriki hao waliokutana wakati walivyoshiriki shindano hilo hadi sasa
katika suala la kisera na changamoto walizokutana.
“Tumekutana leo kwa lengo la
kusisitiza umuhimu wa wazalishaji wadogo wa chakula na kuendelea kusherekea
mafanikio waliokuwa nao kwani zaidi ya asilimia 80 ya chakula uzalishwa na
wazalishaji wadogo wa chakula,”alisema Devotha
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge Kilimo,Mifugo ,Uvuvi na Maji ambae ndio alikuwa mgeni rasmi wa
kongamano hilo, Mh. Mary Nagu alisema kuwa umasikini nchini Tanzania hauwezi
kuisha kama wanawake hawataendelea kupambana katika ujasiriamali, kilimo,uvuvi
na mifugo .
Nagu alisema wanawake wapo wengi
nchini na uwezo wao ni mkubwa katika kukomboa taifa katika kuondokana na
umaskini hivyo ni vema wakasaidiwa na kunyanyuliwa .
Naye Mkurugenzi wa Shirika la
Oxfam nchini ,Francis Odokorach alisema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia
81 ya wanawake nchini Tanzania wamejikita katika kilimo huku wanaume wakiwa
asilimia 73.
“Oxfam ni shirika la kimataifa
linalofanya kazi katika nchi 90,ikiwemo Tanzania,tunaimani kufanikisha
mabadiliko endelevu kwa kuwainua wakulima wanawake wadogo kwa kuwasaidia katika
sekta ya kilimo,”alisema Odokorach
Alisema kutokana na
wanawake kuwa na nguvu katika kilimo,Serikali ingewapa kipaumbele wanawake hao
katika rasilimari zinazohitajika kwani wao ni miongoni mwa watu wanaochangia
pato la taifa.