vingeundwa kizalendo visingembeza Dk Magufuli
Na Mwandishi Wetu , Kigoma
Umoja
wa Vijana wa CCM (UVCCM) umesema upinzani uliopo ni mabaki ya vyama vya
wanasiasa uchwara waliojitahidi kwa miaka mingi kuvipinga Vyama vya
TANU na ASP hatimaye Serikali zake mara baada ya Uhuru wa Tanganyika
mwaka 1961 na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Pia
Umoja huo umesema upinzani wa ulipo nchini hauna chochote cha kupoteza
kwasababu vyama hivyo vimerithi sera na mipango ile ile ya wakoloni na
sultan ya kuwawagawa wananchi, kuwagombaniaha na ikibidi wakiomba hata
damu imwagike.
Msimamo
huo umeelezwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
wakati alipozumgumza na viongozi na wananchma wa ccm kata ya Nguruka
wilaya ya Uvinza Mkoani hapa .
Shaka
alisema baadhi viongozi wa vyama vya upinzani laiti vingelikuwa
vimenazisha kwa ajili ya kupigania maslahi ya umma, kupigania
maendeleo, vikikerwa na umasikini wa watu, ufisadi, rushwa na
ubadhirifu, visingebeza juhudi za serikali ya Rsis Dk John Magufuli.
Alisema
kwasababu viongozi wa vyama hivyo hawajali shime ya uzalendo huku
baadhi yao kuwa nai sehemu ya saratani ya ufisadi na ubadhirifu wa mali
za umma, ndiyo maana hawana jipya kwani hata wanaposhinda serikali za
vijiji ,uwakilishi wa kata na majimbo hushindwa kubuni na kuleta kasi
ya maendeleo.
"Wapinzani
wa sasa ni wale wale warithi wa msimamo ya kuvipinga TANU na ASP ni
mabaki na masalia ya sera za kisultan na ukoloni, hawana jipya ndiyo
maana wanabeza juhudi za serikali ya Dk Magufuli, wangelikuwa wazalendo
na waungwana, wasingeona aibu kumuunga mkono Rais badala ya kumpinga
"Alisema Shaka
Aidha
alisema si hivyo tu lakini pia wapinzani hao hata mchakato na mpango
mkakati wa kuyaunganisha yaliokuwa Mataifa huru ya Tanganyika na
Zanzibar na kuunda muungano, waliupinga na hata sasa wanataka kutugawa
kwa manufaa ya wale wanaowatuma na kuwatumikia
Shaka
alisema vyama hivyo vya zamani ambavyo zimeacha urithi wake kwa vyama
vya upinzani vilivyopo ,havipendi kuona umoja, mshikamano na upendo
ukimarika na kuwanufaisha wananchi kuendelea kuishi pamoja kwa kufuata
sheria na kutii katiba ya nchi.
"Unapovipima
vyama vya upinzani,uwepo wa viongozi wake wanaoshika madaraka kwa miaka
mingi ,sera zake , mipango yao na matamshi wanayotamka, yatamjengea
picha kila mmoja wetu kuviona vyama hivyo vimejaa wanasiasa
wababajishaji wenye malengo ya kusimamia urithi wa sera za kisultan na
kikoloni "Alieleza shaka .
Kaimu
huyo katibu Mkuu wa UVCCM aliwataka wananchi kutambua kuwa Muungano wa
Tanganyika na zanzibar hautakufa kama inavyokusudiwa na na wapinzani
ili kuligawa Taifa na kulisibabishia mitafaruku.
"Kwa
bahati mbaya Rais Dk Magufuli amekwishasema na kuweka
msimamo,atakayejaribu kuusambaratisha muungano atasambaratika yeye kabla
ya kuuyumbusha muungano na watu wake "Alisema Shaka.
Alisema
chama cha mapinduzi kitaendelea kuwatumikia wananachi wake wa Bara na
Zanzobar na kamwe hakuna mtu atakayeturudisha katika zama ya ukoloni au
usultan.