UVCCM YATANGAZA VITA DHIDI YA HALMASHAURI ZOTE NCHINI ZISIZOTOA MKOPO WA ASILIMIA 5 KWA VIJANA

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizungumza wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM, katika ukumbi Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akikagua mradi wa vijana wa umwagiliaji Mtaa wa Imalang'ombe wakati wa ziara ake ya kikazi Katika Manispaa ya Ilemela
 Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manispa ya Ilemela pamoja na Wageni toka nchini Sweeden wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Wilaya ya ilemela
 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akishiriki shughuli ya ufyatuaji tofali kuwaunga mkono vijana wa kikundi kinachodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Anjeine Mabula

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Ilemela Kheri D Jemes  (wa pilikulia)akitoa ufafanuzi katiaka mradi wa vijana wa kufyatua matofali katiak  kikundi kinachodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Anjeine Mabula


  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na vikundi vya wajasiliamali Vjana na kinamama vilivyo nufaika na pesa ya Asilimia 5 kwa vijana na kinamama wilayani ilemela .
 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akifungua rasmi ofisi ya vijana wajasilia mali walionufaika na fedha za asilimia 5 za vikundi katika halmashauri ya wilaya ya ilemela.
 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizindua Shina la wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi katika eneo la Nyehunge
 Shina lililozinduliwa na  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC alipokutana kuzungumza na viongozi na wanachama wa ccm katika Uwanja wa CCM KIRUMBA.
 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) wa pili kulia akivikwa Stafu na Moja wa GREEN GUARD  alipokutana kuzungumza na viongozi na wanachama wa ccm katika Uwanja wa CCM KIRUMBA.
 Wanachama na Viongozi wakipunga mikono
 Mhe Mbunge wa jimbo la ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi akizungumza wakati wa mkutano wa ndani wa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC alipokutana kuzungumza na viongozi na wanachama wa ccm katika Uwanja wa CCM KIRUMBA.
Katibu wa Mkoa wa CCM ndg:akizungumza wakati wa mkutano wa ndani wa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC alipokutana kuzungumza na viongozi na wanachama wa ccm katika Uwanja wa CCM KIRUMBA.
  (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI )


Na Mwandishi Wetu, Mwanza


Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umetangaza kiama dhidi ya Halmashauri zote nchini zisizotoa asilimia 5 ya mikopo kwa Vijana kama ilivyoainishwa na Ilani ya Ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Umoja huo umesema kuwa hakuna Taifa lolote Duniani ambalo linaweza kuajiri Vijana wote badala yake Vijana husaidiwa na Serikali kupitia mbinu Mbalimbali za kuwakwamua kiuchumi ikiwemo kuwapatia mikopo na kuwasaidia kujiajiri.


Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo Julai 24, 2017 Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza Wakati wa ziara ya siku moja alipokuwa akizungumza na Vijana wa Jumuiya ya Chama hicho (UVCCM) pamoja na  wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa ndani uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba.


Shaka alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinafahamu kuwa Changamoto kubwa ya Vijana nchini ni ukosefu wa ajira lakini Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi inaendelea kutumia njia Mbalimbali ikiwemo kuwashauri Vijana Kujiunga na vikundi Mbalimbali ili wapatiwe mikopo waweze kujiajiri wenyewe.


"Nitakuwa muongo kama nitasema sifahamu changamoto zinazowakabili Vijana wengi kiuchumi kwa wale waliopo ndani ya Chama Cha Mapinduzi ama wale waliopo nje ya CCM lakini Serikali inayotekeleza ilani yetu ya ushindi ya Mwaka  2015 imeeleza vyema namna bora ya kuwasaidia Vijana kujiajiri" Alisema Shaka


Alisema kuwa Vijana na watanzania kwa ujumla wake wanapaswa kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli za kuwaletea maendeleo huku akisifu Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kuanza vyema kuwapatia mikopp Vijana wa Manispaa hiyo.


Alisisitiza kuwa Vijana wanapaswa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali, na Vikundi vya uzalishaji Mali, Vitakavyowasaidia wao Vijana, Wanawake na Taifa kwa ujumla kupambana na hali ya kiuchumi katika jamii.


Shaka amewasihi Vijana kurudisha haraka fedha za mikopo pindi wamalizapo matumizi ya fedha hizo ili ziweze kuwasaidia Vijana wengine, zaidi amewasihi Vijana wote kuwa wabunifu kwenye kipato ili waweze kuishawishi Serikali kuwaongeza fedha nyingi katika miradi yao.


Sambamba na hayo pia Shaka amesifu Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela,  sambamba na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kazi kubwa ya kuwashirikisha Vijana katika shughuli za maendeleo wanazozifanya.


MWISHO

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post