Uzinduzi wa albamu ya tatu kutoka kwaya ya
JERUSALEM CITY SINGERS ya Bugarika Jijini Mwanza, unatarajiwa kufanyika jumapili ijayo Julai 23,2017 katika viunga vya Rock/ Kishimba Beach Garden Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa kwaya hiyo, Samwel Maneno amesema hakuna kiingilio katika uzinduzi huo na kwamba shughuli nzima itaanza majira ya saa saba kamili mchana ambapo waimbaji mbalimbali wakiwemo Born To Praise, Voice Of Calvary na Lake Zone watahudumu siku hiyo.
"Hii ni albamu yetu ya tatu ya video iitwayo
MUNGU WA AJABU ambapo imetanguliwa na albamu mbili ambazo ni
DUNIA MAHUTUTI na
HAJAKUSAHAU hivyo nawakaribisha watu wote kushiriki nasi kwenye uzinduzi huo". Amesema Maneno.
[caption id="attachment_27396" align="aligncenter" width="620"]
Usikose uzinduzi huu, ni Jumapili ijayo Julai 23,2017 katika viunga vya Rock/ Kishimba Beach Garden Jijini Mwanza, kuanzia saa saba kamili mchana, ambapo hakuna kiingilio. Wasiliana na Jerusalem City Singers 0758 06 10 44[/caption]
Bonyeza HAPA taarifa zaidi
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia