Na Mwandishi Wetu, kigoma
Umoja
wa Vijana wa CCM (UVCCM)umesema serikali ya awamu ya tano itaendelea
kuwajali na kuwahumiia wagonjwa kwa kupeleka idadi ya waganga, wauguzi,
dawa na utoaji wa vifaa tiba katika zahanati vituo vya afya na hospitali
za wilaya nchini .
Pia
Serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha katika kila Kata na
Wilaya kunajengwa zahanati na vituo vya afya ili kunusuru pia kupunguza
vifo vya kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano .
Msimamo
huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
alipotembelea katika kituo cha Afya cha kijiji cha Nguruka Wilaya ya
Uvinza Mkoani Kigoma katika siku ya pili ya ziara yake kuona utekelezaji
wa ilani ya uchaguzi ya ccm katika maendeleo ya kisekta .
Shaka
alisema serikali ya Chama Cha Mapinduzi zina wajibu wa kufuatilia kwa
karibi na kujua kama yale yote yalioahidiwa katika ilani , yanayotimizwa
na iwapo yanawafikia na kuwahudumia wananchi kama inavyokusudiwa na
serikali Kuu kwa wananchi wake.
Alisema
pamoja na kukabiliwa na upungufu wa idadi ya Waganga na Wauguzi katika
Kituo cha Afya Nguruka, waliopo wamekuwa wakijituma bila kuchoka huku
wakitoa huduma kwa njia makini na sahihi ili kunusuru na kutibu
wagonjwa .
"Serikali ya
CCM katu haitapuuzia dhamana waliopewa na wananchi kwa kuiweka
madarakani kidemokrasia , maeneo yote ya kisekta yataendelea kupata
huduma bora kwa wakati stahili hususan eneo la Afya kwa upelekaji vifaa
tiba, dawa, Waganga na Wauguzi " Alisema Shaka .
Alisema
katika kuonyesha serilali kujali matatizo ya wagonjwa hivi karibuni
Rais John Magufuli amepeleka shilingi milioni kumi katika kituo cha Afya
Nguruka kwa ajili ya kufanyika upanuzi wa wodi ya wazazi huku kanisa
la shalom likijenga wodi hiyo.
"Rais
wetu hapati usingizi kwa raha kutokana na kufikiria wanachi wake, kila
wakati amwkuwa akiwahimiza wataalam wa huduma za afya na watendaji
dhamana wa serikali watimize wajibu wao bila kuchoka. Huuu ndiyo
uungwana alionao kiongozi wetu na kila mmoja wetu sasa lazima awajibike
'Alisema Shaka mara baada ya kutazama wodi hiyo.
Aidha
Kaimu huyo Katibu Mkuu wa UVCCM aliwataka watendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Uvinza kujiongeza katika mikakati ya ubunifu, utendaji
unaoonekana na kujali maisha ya watu, matumizi bora ya fedha za ruzuku
ya umma toka serikali kuu na kuhakikisha wanawatibia wagonjwa kwa wema.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu Msaidizi wa Kituo cha Afya Nguruka Dk Beatrice
Mtasigwa alimueleza Shaka licha kukabiliwa na upungufu wa Waganga na
Wauguzi, wamekuwa wakiwahudumia wagonjwa mbalimbali toka vijiji vyote
wanaofika kituoni kati 80 hadi 120 kwa siku.
Dk
Mtasigwa alisema hatua ya ujenzi na upanuzi wa wodi ya wazazi , uwepo
wa badhi ya vifaa tiba vya kisasa utasaidia kwa kiasi kikubwa kunusuru
maisha ya kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka
mitano.
Naye Mbunge wa
Vijana Mkoa Kigoma Zainab Katimba alitoa shilingi laki mbili na
kumkabidhi Mganga Mkuu Msaidizi wa Kituo hicho cha Afya kusaidia
kununulia shuka ambazo zitatumika katika wodi ya wazazi .
Katimba
alisema bila kina mama hakutakuwa na Taifa kwasbabau nchi na mataifa
yote yanajazwa na nguvu za kina mama ambazo ndiyo wazazi wanaoleta neema
ya kupatikana watoto duniani , wataalam wa fani mbalimbali, viongozi,
wabunge na wanasiasa .
Shaka
anaendelea na ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Kigoma Mjini kabla
ya kuelekea Kibondo, kasulu, Buhigwe, Kakonko na Kigoma vijijini mkoani
hapa