MAANDANDALIZI YA MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA KASKAZINI YAPAMBA MOTO

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera,akifunga kikao cha maandalizi ya sherehe za nane nane, katika viwanja vya maonyesho hayo,jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera amesema maonyesha ya kilimo na mifugo, maarufu kama nane nane mwaka huu kwa kanda ya Kaskazini yataongoza kwa ubora kwa nchi nzima.


Aliyasema hayo alipokuwa akifunga kikao cha maandalizi ya sherehe hizo za nane nane kwa kanda ya Kaskazini ambayo yanajumuisha mikoa mitatu ya Arusha,Manyara na Kilimanjaro.

Amesema kwa Serikali hii ya awamu ya tano niwajibu wakila mtu kufanya kazi kwa bidii nakuacha kufanyakazi kwa mazoea, ili kila mipango iliyowekwa katika maandalizi hayo yafanikiwe na kanda hii kushika nafasi ya kwanza nakua mfano kwa nchi nzima.

Akisisitiza zaidi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameziagiza TANESCO na AUWSA kuhakikisha maji na umeme vinapatikana katika maeneo husika ya viwanja vya maonyesho ya nane nane ndani ya wiki moja.
Pia, Gambo amemwagiza mkuu wa wilaya ya Arusha  kuunda tume yakufuatilia taratibu za matumizi ya viwanja hivyo hasa katika wakati ambao sio wa maonyesho, ili kusaidia kupata taarifa kamili itakayosaidia kutoa hali halisi kabla ya makabidhiano baina ya taasisi iliyokuwa ikisimamia maonyesho hayo TASO na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Gelasius Byakanwa amesema pia katika kikao kijacho nivizuri taarifa ya mapato na matumizi kwa mwaka jana na mwaka huu isomwe kwa wajumbe ili waweze kupata hali halisi ya mapato hayo.

Maonyesho ya nane mwaka huu yataratibiwa na ofisi za makatibu tawala wa mikoa yote mitatu ya kanda ya Kaskazini kwa ushirikiano na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvivu na mpaka sasa ni makampuni  33 tu ndio yamedhibitisha ishiriki katika maonyesho hayo, wananchi wote bado wanahamasishwa kushiriki kuanzia siku ya mwanzo hadi mwisho.

Wakuu wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini wakikagua maandalizi ya maonyesho ya nane nane,jijini Arusha.

Baadhi ya viongozi wa kutoka mikoa ya kanda ya Kaskazini waliohudhuria kikao cha maandalizi ya maonyesho ya nane nane,jijini Arusha.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post