Nabii mkuu Tz Mh Dk. GeorDavie
amewataka watu kuwa na moyo wa kusamehe pale wanapokoseana ikiwa ni pamoja na
kuwa na umoja ili waweze kusimama imara katika maeneo mbalimbali maishani.
Nabii Mkuu Tz Mh Dk. GeorDavie
ameyasema hayo jana katika ibada ya jiji iliyofanyika katika hema la kukutania chuo
kikuu cha manabii kisongo Arusha ambapo ilikuwa siku ya Jumapili ya kusanyiko
Pia katika mafundisho yake Nabii
Mkuu Mh Dk. GeorDavie amewataka watu popote wanapokwenda wasiache kuikumbuka
nguvu ya mungu iliyowainua kwani
nguvu hiyo ndio imekuwa nguzo katika maisha yao
yote.
Aidha, Nabii Mkuu
Mh Dk. Geordavie pamoja na mchungaji kiongozi Mama Anna Davie wanatarajiwa
kuwepo radioni leo majira ya saa mbili na nusu hadi saa tatu na nusu usiku katika kipindi cha kusapoti magurudumu
ya radio.
Pia katika kipindi hicho Mh. Nabii
Mkuu atafafanua kuhusu ujio wake wa Jumapili hemani kisongo, Ratiba ya Pipa day
pamoja na kutamka matamko ya kinabii.