Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angela Kairuki akihutubia kwenye mkutano wa kitaifa wa shukrani na kumuombea Rais Dk.John Magufuli pamoja na nchi uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.
Kwaya ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama ikitoa burudani ya nyimbo za kumsifu mungu katika mkutano huo.
Burudani ya kwaya ikiendelea.
Kikundi cha Utoaji Hamasa kikiwa kazini uwanjani hapo.
Mwonekano katika majukwaa.
Maandamano yakipita mbele ya mgeni rasmi Angela Kairuki.
Maandamano yakiendelea.
Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Jane Magigita akimwelekeza jambo mgeni rasmi wa mkutano huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angela Kairuki baada ya kuwasili kwenye mkutano huo.
Baadhi ya maaskofu na wachungaji wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mratibu wa maombi hayo ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abudant Blessing Center (ABC), Askofu Flaston Ndabila akisalimiana na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Angela Kairuki akisaini baada ya kufika katika mkutano huo.
Wananchi wakiwa jukwaani wakati wa mkutano huo.
Mtumishi wa mungu muhubiri wa kimataifa mtanzania anayeishi Marekani, Dk. Nicku Kyungu 'Mama Afrika' (katikati), akiwa meza kuu na mgeni rasmi, Angela Kairuki (kulia). Kushoto ni Mratibu wa maombi hayo ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abudant Blessing Center (ABC), Askofu Flaston Ndabila
Jukwaani.
Wanafunzi kutoka Shule maalumu ya Jeshi la Wokovu wakiimba katika mkutano huo.
Mtumishi wa mungu muhubiri wa kimataifa mtanzania anayeishi Marekani, Dk. Nicku Kyungu 'Mama Afrika' akizungumza kwenye mkutano huo.
Maaskofu wakimsindikiza mgeni rasmi Angela Kairuki kuelekea jukwaa lililoandaliwa kwa maombi na kuhutubia.
Maombi yakifanyika.
Askofu Bernard Nwaka kutoka nchini Zambia akimuombea Rais Dk.Joh Magufuli.
Mtumishi wa mungu Askofu kutoka Marekani akiomba.
Askofu Timoth Joseph kutoka Nigeria akiombea nchi.
Askofu Sylvester Gamanywa akiomba.
Maombi ya kuombea vyombo vya usalama na ulinzi yakifanyika.
Maombi yakiendelea.
Askofu kutoka Afrika Kusini akiombea nchi.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maombi hayo, Askofu Mkuu wa Naoith Pentekoste Church, Dk.David Mwasota akiombea nchi kuhusu uchumi.
Mtumishi wa mungu muhubiri wa kimataifa mtanzania anayeishi Marekani, Dk. Nicku Kyungu 'Mama Afrika' akiteta jambo na Waziri Angela Kairuki.Mwakilishi wa Askofu Dk. Alex Malasusa wa Kanisa la Kinjili la Kilutheri Tanzania , Mchungaji Andrew King akizungumza kwenye mkutano huo.
Maaskofu Wakuu wakiwa jukwaani katika mkutano huo.
Maombi ya kuombea nchi yakiendelea.
Kwaya ikitoa burudani.
Mratibu wa maombi hayo ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abudant Blessing Center (ABC), Askofu Flaston Ndabila akihitima maombi hayo kwa kutoa neno la shukrani.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI itaendelea kuboresha mazingira bora na wezeshi ili kila mtanzania apate uhuru wa kuabudu kupitia dini yake na hata kwa yule ambaye hana dini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora , Angela Kairuki wakati akihutubia kwenye maaombi maalumu ya kitaifa ya kuombea nchi na Rais Dk.John Magufuli yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana ambapo alikuwa mgeni rasmi.
"Serikali licha ya kuwa haina dini itaendelea kuboresha mazingira ya kuabudu ili kila mwananchi apate fursa ya kuabudu bila ya bugudha yoyote" alisema Kairuki.
Alisema viongozi wa dini kuptia taasisi zao wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuiletea nchi maendeleo na amani ambayo imedumu tangu tupate uhuru hivyo wanapaswa kupongezwa.
Kairuki alisema serikali ina thamini maombi yanayofanywa na viongozi wa dini hapa nchini kwani yanaleta amani, umoja na uzalendo na si kwa waumini wa dini pekee bali na kwa watu wote wenye mapenzi na nchi yetu.
Waziri Kairuki alisema ni vizuri tukatumia fursa hii ya amani iliyopo nchini kwa kila mtu kufanya kazi kwa bidii kama Rais Dk.John Magufuli anavyohimiza kila siku ikiwa pamoja na kumuombea.
Mtumishi wa mungu muhubiri wa kimataifa mtanzania anayeishi Marekani, Dk. Nicku Kyungu 'Mama Afrika' ambaye alipata maono ya kufanya mkutano huo wa maombi ya shukrani hapa nchini alisema Afrika pamoja na Tanzania zimebarikiwa kwa kuwa na rasilimali za kutosha tulizopewa na mungu hivyo hatuna budi kumshukuru mungu.
Alisema Tanzania imejaa kila kitu kizuri, mbuga za wanyama, madini, ardhi ikiwemo amani iliyodumu tangu utawala wa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na sasa Dk. John Magufuli.
Alisema kutokana na neema hiyo kutoka kwa mungu aliona ni vema yakafanyika maombi ya shukrani ya kitaifa na kumuombea Rais Dk.John Magufuli na nchi kwa ujumla.
Dk.Kyungu alisema kauli alioianzisha Rais Dk. Magufuli ya Hapa Kazi tu ipo katika biblia hivyo ni wajibu wa kila mtu kufanya kazi kama mungu alivyomuagiza adamu pale bustani ya hedeni na hiyo itasaidia kupambana na adui umaskini, ujinga na maradhi hasa katika kipindi hiki ambacho Rais Dk. John Magufuli anahimiza nchi kuingia katika uchumi wa viwanda.
Katika maombi hayo maaskofu wakuu zaidi ya kumi kutoka ndani na nje ya Tanzania waliweza kuiombea nchi katika maeneo mbalimbali, kama uchumi, vyama vya siasa na viongozi wao, Rais na Serikali, Bunge, amani, masuala ya ulinzi na usalama na mambo mengine.
Maombi hayo ambayo ni ya kihistoria hapa nchini yaliandaliwa na viongozi wa dini kutoka madhehebu ya Huduma ya Kikristo Tanzania na Taasisi ya I Go Africa For Jesus yalifanyika kuanzia saa nne asubuhi hadi jioni na kuhudhuriwa na mamia ya watanzania na viongozi wa dini huku yakipambwa na burudani za nyimbo za kumtukuza mungu kutoka kwaya mbalimbali ambapo yalifungwa na neno la shukrani na Mratibu wa maombi hayo ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abudant Blessing Center (ABC), Askofu Flaston Ndabila.
Baadhi ya maaskofu wakuu waliohudhuria maombi hayo ni pamoja na Dk. Philemon Tibananason, Dk.Bernard Nwaka kutoka Zambia, Sylvester Gamanywa, Lawrence Kameta, Dk.Barnabas Mtokambali, Timoth Joseph kutoka Nigeria na wengine kutoka nje ya nchi.